loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Tuwe makini kuepuka majanga

KATIKA gazeti letu la leo tumeandika kwamba, familia zenye idadi ya watu 1,655 zimekimbia nyumba zao baada ya Ziwa Tanganyika kujaa maji na kusababisha mafuriko makubwa katika kijiji cha Kipwa, wilaya ya Kalano, mkoani Rukwa.

Kwenye habari hiyo imeelezwa kwamba, takribani nyumba 180 zimebomolewa na mafuriko hayo.

Katika mazingira ya kawaida, unaposoma taarifa hii simanzi inakujia na haraka unatafuta namna ya kusaidia jamii hii ili isiadhirike.

Pamoja na kuwapa pole wananchi walioathirika kutokana na kufurika kwa Ziwa Tanganyika, lakini pia kuna funzo hapa, ambalo tunahitaji kuliangalia kwa undani zaidi na kutengeneza maarifa yanayofaa kwa maisha ya baadae katika maeneo hayo.

Zipo taarifa kuwa, ujenzi wa nyumba hizo ulifanyika katika maeneo makavu ambayo miaka 30 iliyopita maji ya Ziwa Tanganyika yalikuwa yanatamalaki. Kwa maneno mengine, watu hawa wamejenga katika ziwa na mamlaka za maeneo hayo ziliwaacha kuendelea na maisha.

Hatuwezi kujua sababu za kuwapo kwa kijiji hicho katika eneo ambalo zamani lilikuwa na maji, huenda shughuli za uvuvi ndizo zilizaa kijiji hicho na maji yalipopungua ziwani taratibu watu wakalitwaa eneo lililoonekana kuwa kavu na kuwa kijiji.

Kwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Kalambo, Julieth Binyura, amesema mafuriko hayo yaliyokikumba kijiji cha Kipwa yalianza kidogo kidogo tangu Februari, mwaka huu, ambapo Machi, mwaka huu wakazi 450 walikosa makazi baada ya nyumba zao zipatazo 90 kubomoka, ipo haja ya wataalamu kuwaambia ukweli watu wa eneo hili waondoke.

Bila ya kumung’unya maneno, maofisa wa serikali waliokuwa wanatakiwa kutoa vibali mbalimbali walifanya hivyo bila kuangalia ukweli kuhusu Ziwa Tanganyika na mwenendo wake.

Kwa kuwa maji ya Ziwa Tanganyika yanaendelea kujaa na kusababisha mafuriko hadi kijiji chote kufunikwa na maji, ni dhahiri kwamba, waliohusika na kutoa ruksa watu waendelee kutengeneza makazi eneo hili wanahitajika kuhojiwa.

Ni kweli ni kawaida ya binadamu kuhakikisha anakaa eneo ambalo ni karibu na mahitaji yake iwe kilimo au ufugaji au uvuvi, lakini mamlaka zinazohusika na maeneo hayo kuendelea kutoa ruksa ya kuwapo kwa makazi na kupeleka huduma wakati wanajua ni maeneo hatarishi, haiwezi kuingia akilini na haikubaliki.

Tunasema haiwezi kuingia akilini kwa kuwa kila kitu kinajulikana na bila sababu yoyote ya msingi wahusika wanaacha kuwabana watu kisheria ili kupunguza madhara yanayoambatana na kuwa katika eneo ambalo ziwa linapumulia linapokuwa pomoni.

WIKI hii kumekuwa na taarifa za Yanga kutakiwa ...

foto
Mwandishi: Mhariri

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi