loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Ondoeni hofu corona inapita tu

RAIS John Magufuli jana alihutubia taifa kwa mara nyingine na kuendelea kuwataka wananchi kuacha hofu kwa ugonjwa wa homa ya mapafu, covid 19 inayosababishwa na virusi corona.

Ametoa rai hiyo wakati akihutubia kutoka kwake Chato mkoa wa Geita baada ya kumwapisha Waziri mpya wa Katiba na Sheria, Dk Mwigulu Nchemba aliyechukua nafasi ya Dk Agustine Mahiga aliyefariki na kuzikwa juzi mjini Iringa.

Tunaungana na wananchi kumpongeza kwa mara nyingine, Rais Magufuli kwa kuongoza vyema vita dhidi ya corona akiwa mstari wa mbele kwa kuwatia moyo Watanzania wote.

Ni ukweli usiopingika kuwa kutokana na virusi vya corona kutoonekana, watu wengi nchini wamekuwa wakiishi kwa hofu ya kuambukizwa na kufanya wengine washindwe kufanya kazi.

Ni kutokana na ukweli huo, hotuba ya jana ya Rais Magufuli imekuja wakati muafaka ambapo vita hii inashika kasi huku watu wengi nchini wakihamasishwa kujilinda na kujikinga zaidi.

Kwamba Rais Magufuli amefichua mambo ya kushangaza kuhusu vipimo vya waathirika wa corona kuonesha utata baada ya sampuli za mapapai, mbuzi, mafenesi, oli chafu, kwale kuchukuliwa na kutoa majibu yenye kutia shaka inaacha maswali mengi kuhusu ugonjwa huu.

Ni kwa sababu hiyo, tunaungana naye kutaka wananchi kuchukua tahadhari kubwa lakini pia kuondoa hofu kwa sababu corona inaonekana ina siasa zilizofichika hivyo tusimame imara.

Kwa mfano, Rais Magufuli alihoji usahihi wa vipimo vinavyotumika kupima ambavyo ni vya kutoka nje na njia zinazotumika kupima akitoa changamoto kwa wanasayansi wa mashirika ya afya kama WHO na wasomi kuchambua zaidi.

Ni kwa sababu hiyo tunasema, badala ya kukaa tu na kukubali kushindwa na corona, umefika wakati wa kila Mtanzania kusema hapana kwa ugonjwa huo kwa kuzingatia miongozo ya afya huku wakimwomba Mwenyezi Mungu asaidie.

Tuonavyo sisi, Tanzania kama ilivyo kwa nchi nyingine duniani, ina nafasi kubwa ya kushinda vita hii kama wananchi watajitoa mhanga katika kupambana na kuenea kwa maambukizi yake.

Wafanye hivyo kuunga mkono hatua za serikali kupambana na ugonjwa huo likiwemo la kuagiza dawa kwa ajili ya tiba kutoka Madagascar na kuacha kutishana kuhusu kiwango cha maambukizi.

WIKI hii kumekuwa na taarifa za Yanga kutakiwa ...

foto
Mwandishi: Mhariri

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi