loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Shule za msingi, sekondari sasa kufunguliwa Septemba

WIZARA ya Elimu imesema shule za msingi na sekondari zitafunguliwa Septemba, mwaka hu una kuwaondoa hofu walimu na wanafunzi kuwa shule hazitafunguliwa mwaka huu.

Uamuzi huo umetolewa na baraza la mawaziri katika kikao chake cha kutathmini mapambano ya kudhibiti virusi vya corona vinavyosababisha ugonjwa wa covid-19. Waziri wa Elimu, Teknolojia ya Mawasiliano na Elimu ya Ufundi, Claudette Irere, alisema taasisi nyingine za elimu zitafunguliwa baada ya wanafunzi wa shule za msingi na sekondari kuanza masomo.

“Kwa taasisi za elimu tunafahamu kuwa wapo waliobakiza miezi michache kumaliza mwaka wa masomo, hivyo watarejea vyuoni mara baada ya shule za msingi na sekondari kufunguliwa,” alisema.

Alisema walimu wa shule za umma wataendelea kupata mishahara yao ya mwezi kwa sababu wanaendelea kusaidia wanafunzi kupitia mifumo mbalimbali ya mafunzo.

“Kwa walimu wa taasisi binafsi, ambao wameathirika sana wakati huu, tunataka wamiliki wa taasisi hizo kutafuta misaada katika mifuko ya serikali ya kusaidia sekta binafsi ili waendelee kuwalipa walimu wao,” alisema.

Kuhusu wazazi waliolipa ada, Irere alisema hakutakuwa na kurejeshwa ada, kwani janga hilo limeathiri watu wengi na kwamba muda huu mpaka Septemba utatumika kujenga madarasa zaidi ili wanafunzi watakapofungua shule kuwe na uwiano mzuri baina ya walimu na wanafunzi.

foto
Mwandishi: KIGALI

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi