loader
Picha

Mahabusu zaidi ya 1,600 waachiwa

MAHABUSU 1,673 wameachiwa huru kutoka katika vituo mbalimbali vya polisi nchini, ili kukabiliana na mikusanyiko katika maeneo hayo na kudhibiti maambukizi ya virusi vya corona vinavyosababisha ugonjwa covid-19.

Idadi hiyo ya mahabusu walioachiwa huru ni kubwa tangu ulipoanza utaratibu wa kuwaachia huru maabusu ulioanza mwezi uliopita kwa ushirikiano wa mamlaka ya taifa ya kurekebisha wafungwa (NPPA), Mahakama, Polisi na Taasisi ya Uchunguzi Rwanda.

Mwendesha Mashtaka Mkuu wa Serikali, Aimable Havugiyaremye, mwishoni mwa wiki alisema mahabusu wanaoachiwa huru wako katika vigezo vya aina mbili, wenye makosa wanayoweza kutozwa faini bila kuendelea na kesi na washtakiwa watakaoachiwa kwa sababu mbalimbali. Hata hivyo, alisema walioshatakiwa kwa makosa makubwa hawatanufaika na msamaha huo.

Msemaji wa NPPA, Faustin Nkusi, alisema msamaha huo utaendelea, kwani ingawa kumekuwa na zuio la serikali la watu kutoka nje, kuna baadhi ya watu wanaendelea kufanya makosa na kupelekwa vituo vya polisi. Nkusi alisema walioachiwa huru wamepewa masharti mbalimbali, ikiwamo kutokwenda baadhi ya maeneo.

NCHI za Tanzania na Kenya zimeafikiana kuwa madereva ...

foto
Mwandishi: KIGALI

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi