loader
Picha

Wafanyabiashara sokoni kuuza kwa zamu kuepuka corona

WAZIRI wa Viwanda na Biashara, Soraya Hakuziyaremye, amesema wafanyabiashara sokoni watafanyakazi kwa awamu, ili kuepusha misongamani kwenye masoko na kudhibiti kusambaa kwa virusi vya corona.

Uamuzi huo ni kati ya maamuzi yaliyofanywa na baraza la mawaziri katika kurahisisha zuio la watu kutoka nje na kuhakikisha umbali wa mita moja baina ya wafanyabiashara unazingatiwa, huku shughuli nyingine zikiruhusiwa kuanzia jana.

“Masoko yatafunguliwa kwa wanaouza bidhaa muhimu ambao watauza kwa awamu kwa kila awamu kuwa na asilimia 50 ya wafanyabiashara waliosajiliwa,” yanaeleza sehemu ya maelekezo yaliyotolewa na Waziri Mkuu, Edouard Ngirente.

Watakaoruhusiwa ni wafanyabiashara wa bidhaa muhimu kama chakula, dawa na bidhaa za usafi, lakini biashara za bidhaa nyingine kama vifaa vya ujenzi na mavazi hazitaruhusiwa katika masoko.

Hakuziyaremye alisema licha ya kufanya kazi kwa awamu ili kuondoa misongamano na kukaaa umali wa mita moja kati ya mfanyabiashara na mfanyabiashara, pia watatakiwa kuvaa barakoana na glavu bila kukosa ili kujilinda na maambukizi ya virusi vya corona.

NCHI za Tanzania na Kenya zimeafikiana kuwa madereva ...

foto
Mwandishi: KIGALI

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi