loader
Picha

Kampeni za uchaguzi mkuu zapamba moto

KAMPENI kwa ajili ya Uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani unaotarajia kufanyika Mei 20, mwaka huu, zinaendelea kupamba moto baada ya kuzinduliwa rasmi.

Rais anayemaliza muda wake, Pierre Nkurunziza (pichani) na mgombea wa chama tawala CNDD-FDD, Evariste Ndayishimiye, walizindua kampeni ya chama hicho wiki iliyopita katika Jimbo la Gitega, katika eneo la Bugendana.

Ndayishimiye ambaye ni Katibu Mkuu wa chama hicho, alimpongeza Rais Nkurunziza kwa kuimarisha ulinzi na usalama katika nchi hiyo. Alihaidi kufuata nyayo za Rais huyo kuendeleza sekta ya kilimo, rasilimali za asili, ujenzi wa viwanda vya kusindika mazao, kusaidia wawekezaji na kuimarisha uchumi wa nchi.

“Sitalala kama watoto wa Burundi hawapati elimu bora na huduma bora za afya,” alisema Ndayishimiye.

Naye, mgombea wa chama kikuu cha upinzani cha National Congress for Liberty (CNL), Agathon Rwasa, alizindua kampeni zake katika eneo la Ngozi, ambalo ni jimbo alilozaliwa.

Alisema aliahidi endapo atachaguliwa kuwa rais, ataimarisha sekta binafsi, kupambana na umasikini, kupunguza kiwango cha watu wasio na ajira na kuimarisha mahusiano ya kidiplomasia kati ya Burundi na nchi nyingine.

Mgombea urais wa chama cha Uprona, Gaston Sindimwo, alizindua kampeni zake katika jimbo la kati la Mwaro, huku mgombea wa chama cha Frodebu, Léonce Ngendakumana, akizindua kampeni zake katika eneo jirani la Kinama ba mgombea binafsi, Dieudonné Nahimana, alianza kampeni zake Kinindo, Kusini mwa mji mkuu, Bujumbura.

Muungano wa kisiasa wa Kira-Burundi ulizindua kampeni katika Jimbo la Muramvya na mgombea mwingine binafsi, Francis Rohero, alizindua kampeni zake katika kiwanja cha mpira cha Tempête. Bujumbura.

NCHI za Tanzania na Kenya zimeafikiana kuwa madereva ...

foto
Mwandishi: BUJUMBURA

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi