loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Benki ya Dunia kusaidia kaya 65,000

BENKI ya Dunia imethibitisha kutoa dola za Marekani milioni 40 kusaidia kaya 65,000 zenye uhitaji chini Sudan Kusini. Fedha hizo kutoka Taasisi ya Maendeleo ya Kimataifa katika Benki ya Dunia, ni mradi wa miaka miwili na nusu wa kusaidia takribani raia wa Sudani Kusini 430,000.

Msaada huo utatolewa kwa kaya zenye watu wenye uhitaji mkubwa, ikiwamo walemavu, wazee, wajawazito na wanaoishi na virusi vya ukimwi. Mradi huo unatekelezwa na Ofisi ya Huduma za Miradi katika Umoja wa Mataifa (UNOPS) nchini Sudan Kusini, kwa kushirikiana na Wizara ya Kilimo na Chakula, Wizara ya Jamii na Jinsia na Wizara ya Fedha na Mipango.

Taarifa ya UNOPS ilisema mradi huo utasaidia kutoa huduma muhimu na fursa za mapato na ajira za muda. “Ninashukuru Sudan Kusini kupata fedha za ziada zitakazotumika kujenga miradi kwa wahitaji,” alisema Waziri wa Kilimo na Chakula, Josephine Lagu.

Alisema fedha hizo pia zitatumika si tu kuboresha usalama wa chakula kwa maelfu ya watu, lakini pia kuongeza uimara wa uchumi. Mwakilishi Mkazi wa UNOPS nchini Sudan Kusini, Peter Mutoredzanwa, alisema taasisi hiyo itaendelea kufanya kazi kwa karibu na Benki ya Dunia, serikali na wadau wengine kutoa huduma muhimu, kuboresha maisha na kukuza maendeleo.

foto
Mwandishi: JUBA

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi