loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Museveni aitaka EAC kushikamana vita ya Corona

RAIS wa Uganda, Yoweri Museveni, amesema nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) hazikuwa na sababu ya kuendelea kuteswa na virusi vya corona kama itifaki zote zingetekelezwa kwa pamoja na kwa wakati.

Amesema lengo la kuundwa kwa jumuiya hiyo ni kurahisisha utatuzi wa changamoto zinazokabili nchi moja moja wanachama au zinazokabili mataifa yote kwa wakati mmoja kama ilivyo sasa ugonjwa wa Covid- 19.

Kiongozi huyo mkongwe kuliko wote katika nchi za EAC), alisema changamoto zinazoikabili Kanda ya Afrika Mashariki zinahitaji utatuzi au nguvu ya pamoja ili kuzishinda.

“Tungeshikamana vizuri kusingekuwa na mgogoro wa Sudan Kusini, kusingekuwa na mgogoro wa kisiasa nchini Burundi wala kusingekuwa na shida inayosababishwa na virusi vya corona,” alisema.

Rais Museveni alisema kinachopaswa kufanywa ni kuzingatia nia ya waasisi wa mataifa hayo na Jumuiya ya Afrika Mashariki kwa ujumla.

“Tukiwa pamoja hatutateswa na corona, tukiwa pamoja hatutateswa na njaa, tukiwa pamoja hatutateswa na nzige,” alisema Rais Museveni.

foto
Mwandishi: KAMPALA

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi