loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Watumishi waliokufa ajalini watajwa

WATU watatu kati ya hao wawili wakiwa ni watumishi wa Idara ya Afya mkoani Singida, wamefariki dunia baada ya gari walilokuwa wakisafiria aina ya Toyota LandCruiser Hardtop kugongana uso kwa uso na basi la Kampuni ya Happy Nation, Feri Dumila wilayani Kilosa mkoani Morogoro kwenye barabara kuu ya Dodoma – Morogoro.

Kamanda wa Polisi mkoani Morogoro, Wilbroad Mutafungwa alisema jana kuwa ajali hiyo ilitokea Mei 5, mwaka huu saa mbili usiku eneo la Feri, Kata ya Dumila, Tarafa ya Magole wilayani Kilosa.

Kamanda Mutafungwa alisema gari aina ya Higher yenye namba za usajili T483 DRF mali ya Kampuni ya Happy Nation ikitokea Mwanza kwenda Dar es Salaam, likiendeshwa na Isack John wa Dar es Salaam, iligongana uso kwa uso na gari aina ya Toyota LandCruiser yenye namba za usajili STL 6995 mali ya Idara ya Afya mkoani Singida.

Alisema gari aina ya Toyota LandCruiser, lilikuwa likiendeshwa na Baptist Beda (37) ambaye ni mkazi wa Singida na lilikuwa likitoka jijini Dar es Salaam kwenda mkoani humo.

Aliwataja waliofariki dunia ni dereva wa Toyota Land Cruiser, Beda na abiria mwingine, Guhacha Kitinda (60) ambaye pia ni mkazi wa Singida ambaye ni mtumishi wa serikali mkoani humo, na Sabinaeva Guhacha pia wa Singida.

Kamanda Mutafungwa alisema katika ajali hiyo, Michael Matonya (20) mkazi wa Kibaigwa ambaye alikuwa abiria wa pikipiki aliyejeruhiwa na amelazwa Hospitali ya Mtakatifu Joseph iliyopo Dumila.

Alisema chanzo cha ajali ni dereva wa basi, kujaribu kuipita pikipiki iliyokuwa mbele yake bila kuchukua tahadhari.

Alisema mtuhumiwa ambaye ni dereva wa basi wa Happy Nation, alitoroka baada ya kutokea kwa ajali hiyo na Polisi inaendesha msako mkali ili kumtia mbaroni na kufikishwa mahakamani.

Alisema miili ya marehemu hao, imehifadhiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Morogoro.

MGOMBEA Urais wa Chama ...

foto
Mwandishi: John Nditi, Morogoro

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi