loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

IATA wajipanga kurejesha safari za ndege

SHIRIKA la Kimataifa la Usafi ri wa Anga(IATA), limesema linaendelea kuzungumza na nchi mbalimbani duniani kuangalia uwezekano wa kuanza tena safari za ndege za kimataifa, kwani imebainika kuwa, uwezekano wa abiria kupata maambukizi ya virusi vya corona wakiwa ndani ya ndege ni mdogo.

Aidha, IATA imesema tayari wameshaandaa utaratibu mpya wa matumizi ya usafiri huo wa anga ambapo abiria wote kuanzia sasa watapaswa kuvaa barakoa wakati wote wa safari, sambamba na watoa huduma ndani ya ndege na pia huduma kwa abiria zilizokuwa zinatolewa wakati wa safari ikiwemo vinywaji na chakula hivi sasa vitakuwa vinawekwa kwenye kila kiti cha abiria kabla ya abiria kupanda kwenye ndege.

Akizungumzia uamuzi huo, juzi mjini Geneva Afisa Mtendaji Mkuu wa IATA, Alexandre de Junaic (pichani) alisema jumuiya ya kimataifa za usafiri wa anga zimeendelea kuangalia hatua za kuchukua ili kuhakikisha kwamba usafiri huo unarejea kwa kuzingatia tahadhari ya ugonjwa wa virusi vya corona.

Alisema katika kuhakikisha usafiri huo unakuwa salama na kutokuwa sehemu ya maambukizi ya virusi hivyo kwa abiria, hatua kadhaa zimechukuliwa ikiwa ni pamoja na timu ya wataalamu wa afya wa shirika hilo kutoa muongozo wa jinsi ya kutoa huduma katika usafiri wa anga.

Junaic alisema hatua mojawapo itakayofanywa wakati usafiri huo utakaporejea tena ni kuhakikisha abiria wote pamoja na watoa huduma kwenye mashirika ya ndege kuvaa barakoa wakati wote wa safari.

Aidha, huduma zilizokuwa zikitolewa ndani ya ndege kama vile vinywaji,chakula na huduma ya kwenda maliwato zimewekewa utaratibu maalumu ambapo sasa vinywaji na chakula vitakuwa vinawekwa kwenye kiti cha kila abiria kabla ya abiria kuruhusiwa kuingia ndani ya ndege. Pia, huduma ya kwenda maliwato haitakuwa huru kwa abiria kwenda wakati wowote apendao, bali watalazimika kwenda sio zaidi ya mara mbili huku pia huduma nyingine ndani ya ndege zikipunguzwa ili kuepuka uwezekano wa kuambukizana virusi vya corona.

“Uwezekano wa abiria kupata maambukizi ndani ya ndege ni mdogo, na ndio maana tumeweka utaratibu mpya wa wasafiri na watoa huduma ndani ya ndege mara usafiri huu utakapoanza tena , pia watoa huduma ndani ya ndege hawatakuwa wakipitapita tena kuhudumia, huduma nyingi zitawekwa kabla ya safari kuanza kama vile vinjwaji na vyakula, kila kiti cha abiria kitakuwa na vitu hivyo na abiria atavikuta pindi aingiapo,”alisema Junaic.

Hatua nyingine zilizotangazwa kuchukuliwa pindi usafiri huo urejeapo ni kuhakikisha wanawapima joto wasafiri ,watoa huduma kwenye viwanja vya ndege na watoa huduma wengine wa viwanja vya ndege,kupunguza mizunguko ndani ya ndege kwa watoa huduma na abiria na kuongeza ufanyaji usafi wa mara kwa mara wakati wa safari.

Aidha pia wanaangalia uwezekano wa wasafiri kuwa na kinga kwenye pasi ya kusafiria inayoonesha msafiri yuko salama dhidi ya maambukizi ya corona na anaweza kusafiri. Hata hivyo alisema suala umbali kati ya abiria mmoja na mwingine ndani ya ndege hilo bado ni gumu kwani sio rahisi kuacha wazi viti vya katikati bila kuwa na abiria, vinginevyo gharama zitaongezeka maradufu iwapo hilo litatekelezwa na kuacha maelfu ya abiria wakilia na ukubwa wa gharama za nauli.

“Mambo ya msingi ya kutekelezwa ni hayo niliyozungumzia , lakini suala la umbali wa mita moja kati ya abiria na abiria kwenye ndege ni gumu, ukisema hivyo ina maana viti vyote vya katikati visiwe na abiria, ndege itapata hasara labla gharama ziongezeke na nauli, jambo ambalo ni maumivu kwa wateja, lakini cha msingi ni kwamba uwezekano wa kupata maambukizi ndani ya ndege ni mdogo sana,”alisisitiza Junaic.

Akizungumzia kushuka kwa mapato kwenye sekta hiyo katika kipindi hiki cha mlipuko wa COVID-19, Junaic alisema mashirika ya ndege yanapita wakati mgumu hasa baada ya mlipuko wa corona

WAOKOAJI nchini Lebanon wanatafuta zaidi ya watu 100 waliokufa na ...

foto
Mwandishi: GENEVA,Uswisi

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi