loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Trump atumia kura ya VETO

RAIS wa Marekani Donald Trump ametumia kura yake ya veto kuzuia muswada wa sheria uliokuwa na lengo la kuweka kikomo uwezo wake wa kuanzisha vita na Iran, huku kukiwa na wasiwasi ya kuzuka vita kati ya nchi hizo mbili.

“Ilikuwa azimio la dharau kwa kweli, lililoletwa bungeni na wabunge wa Chama cha Democratic kama sehemu ya mkakati wa kushinda uchaguzi wa Novemba 3 kwa kukigawa Chama cha Republican,” alisema Rais Trump.

Kwa kujibu wa taarifa iliyotolewa Ikulu ya nchi hiyo, Rais Trump alinukuliwa akisema :, “Wabunge wachache kutoka Chama cha Republican waliopigia kura muswada huo wa sheria walijiingiza kwenye mambo wasiyoyajua,”.

Baraza la Seneti, ambapo maseneta kutoka Chama cha Republican ndio wengi, lilitarajiwa kupiga kura jana ya kufuta kura hiyo ya VETO iliyotolewa na Rais Trump. Maseneta wachache kutoka Chama cha Republican na wabunge wa chama hicho katika Baraza la Wawakilishi ambao ni wengi ndani ya Chama cha democratic walipigia kura muswada huo wa sheria mapema mwaka huu.

Itakuwa vigumu kuamini kwamba wingi wa theluthi mbili zinazohitajika katika Seneti zitapatikana kwa kuweza kufuta kura ya turufu ya rais.

WAOKOAJI nchini Lebanon wanatafuta zaidi ya watu 100 waliokufa na ...

foto
Mwandishi: WASHINGTON,Marekani

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi