loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Benjamin Nyetanyahu kuunda serikali

MAHAKAMA Kuu ya nchini Israel, imetoa uamuzi kuwa mashitaka ya ufi sadi dhidi ya Waziri Mkuu wa nchi hiyo, Benjamin Netanyahu hayamzuii kuunda serikali na kwa uamuzi huo sasa unatoa nafasi ya kiongozi huyo wa chama cha Likud kubaki madarakani.

Makundi ya upinzani yaliwasilisha mashitaka katika Mahakama Kuu ya nchi hiyo yakishtumu makubaliano yaliyofikiwa mwezi uliopita kati ya kiongozi huyo Benjamin Netanyahu na hasimu wake mkuu Benny Gantz kwa lengo la kuunda serikali ya umoja wa kitaifa ili kulindoa taifa hilo kwenye mgogoro wa kisiasa ambao haujawahi kutokea katika nchi hiyo.

Makundi hayo yalikuwa yamebaini kwamba mashtaka ya ufisadi, udanganyifu, uvunjaji wa uaminifu yanayomkabili Netanyahu, yangemzuia kuendelea kubaki madarakani. Mahakama Kuu imebaini kwamba makubaliano hayo hayakiuki sheria na kwa hivyo imekataa kuyafuta, ikiondoa kizingiti muhimu kwa muungano wa serikali ambayo Netanyahu na Gantz wanapanga kukubaliana wiki ijayo.

Uamuzi wa mahakama unakuja wakati uchaguzi wa wabunge uliofanyika mara tatu chini ya mwaka mmoja, ambapo uchaguzi wa mwisho ulifanyika Machi 2, pande zote zilishindwa kupata viti vingi bungeni.

Majaji 11 wa Mahakama Kuu wameeleza kwamba uamuzi wao huo “haupaswi kufasiriwa kama kupuuzia uzito wa mashtaka” dhidi ya Netanyahu, na kuongeza kwamba alikuwa na haki ya kudhaniwa kuwa hana hatia. Kesi dhidi ya Netanyau imepangwa kuanza Mei 24 mwaka huu.

WAOKOAJI nchini Lebanon wanatafuta zaidi ya watu 100 waliokufa na ...

foto
Mwandishi: TEL AVIV,Israel

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi