loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Siku ya Mama leo apewe zawadi inayomliwaza

LEO ni Siku ya Mama. Ni siku ya kuadhimisha thamani ya mama na nafasi yake katika jamii. Inatajwa kuwa ni siku ya ukaribu kati ya mama na watoto. Haijalishi ni mama mzazi au mlezi, lengo ni kuadhimisha nafasi ya umama katika maisha.

Siku ya Mama huadhimishwa Jumapili ya pili ya Mei. Asili ya maadhimisho haya ni Marekani, mapema miaka ya 1900. Mwaka 1905 Mwanamke aitwaye Anna Jarvis alianza kampeni kwa ajili ya kurasimisha maadhimisho ya siku ya mama na ndiyo mwaka ambao mama yake mzazi alifariki.

Ilianza kuadhimishwa kwa kiwango kikubwa mwaka 1908 pale ambapo Jarvis alifanya kumbukumbu ya wazi ya mama yake katika mji wa Grafton, West Virginia.

Baada ya miaka michache, Jarvis alishinikiza itambulike kuwa siku ya mapumziko na ilianza kusherehekewa zaidi katika majimbo mbalimbali nchini Marekani. Mwishowe, mwaka 1914, Rais Woodrow Wilson alisaini tamko la kuifanya maadhimisho ya Siku ya Mama yawe rasmi na yafanyike Jumapili ya pili ya Mei.

Anna Jarvis aliweka Siku ya Mama kwenye kalenda kuwa siku maalumu ya kuonesha upendo na shukurani kwa mama wote, kutambua wanavyojitoa mhanga kwa ajili ya watoto.

Duniani kote, siku hi husherehekewa kwa njia mbalimbali na hata tarehe mbalimbali. Lakini kwa Marekani leo ndiyo siku ambayo huadhmishwa ikidhihirisha juhudi zilizofanywa na Anna Jarvis kuifanya itambulike.

Maua, mishumaa na kadi zilitumika kama sehemu ya kuadhimisha siku hii. Hata hviyo katika siku za mwanzoni, Jarvis aliona kama siku hiyo imekuwa ya kibiashara kutokana na kutekwa na watengeneza maua, mishumaa na kadi hivyo kutishia kuharibu mantiki ya siku hii ambayo ilipaswa iwe ya mtu binafsi; kwa maana ya muunganiko kati ya mama na watoto wake.

Kuanzia mwaka 1920 onward, Jarvis alipambana vikali kuzuia wafanyabiashara kujinufaisha na Siku ya Mama kupitia kadi, maua, mishumaa na zawadi. Hata hivyo haikuwa rahisi kutenganisha siku hii na biashara kutokana na ukweli kwamba miongoni mwa vitu ambavyo watu waliwapa mama zao ni pamoja na maua ambayo ili kuyapata ni lazima uyanunue.

Inaelezwa kwamba mwaka 2017, kiwango kilichotarajiwa kutumika kwa aijli ya kuadhimisha siku hii katika Marekani ilikuwa dola za Marekani bilioni 23.6 sawa na wastani dola za Marekani 186.39 kwa kila anayefanya manunuzi.

Kama unataka kufuata njia ya Anna Jarvis, una namna mbalimbali ya kuadhimisha siku hii na kumuenzi mama kwa namna tofauti. Unaweza kumwandikia mama yako ujumbe murua ukamburudisha moyo wake.

Kupiga simu ni njia nyingine ya kujiuganisha na mama katika siku hii hususani kwa walio mbali; kudhihirisha ulivyo karibu naye na unavyothamini mchango wa malezi yake kwako.

Wapo watu au familia zinazofuatilia siku hii na kuiadhimisha kwa namna tofauti wakiwapo waliozoea kuwachukua mama zao na kufanya matembezi kwenye sehemu tulivu na kujipatia chakula au kinywaji.

Lakini katika kipindi hiki ambacho nchi na dunia nzima inapambana na maambukizi ya virusi vya corona, si wakati wa familia kwenda matembezini. Badala yake, familia zikae ndani zile, zinywe pamoja kwa kuzingatia tahadhari zote dhidi ya maambukizi ya virusi vya corona vinavyosababisha ugonjwa wa homa ya mapafu (Covid-19).

Zaidi ya kukaa na kufurahi, siku hii itumike kuwapa moyo na kuwaondolea hofu na taharuki mama wote. Sote tunafahamu mama ndiyo nguzo ya ustawi wa familia.

Kwa hiyo miongoni mwa ujumbe ambao kila mtu anapaswa ampe ‘Mama wa maisha yake’ ni pamoja na usiomtia wasiwasi kupita kiasi dhidi ya Covid-19 asije kupoteza mwelekeo wa kuijenga familia.

Haitoshi kumpa zawadi ya vitu na fedha. Zawadi kuu anayostahili katika siku yake leo ni pamoja na ujumbe uliojaa upendo wa dhati utakaomliwaza na kumpa faraja.

Kwa jumla, siku zote tuendelee kuenzi maono ya muasisi wa Siku ya Mama (Anna Jarvis) kila mmoja aoneshe upendo na shukurani kwa mama wote akitambua wanavyojitoa mhanga kwa ajili ya watoto na familia.

KATIKA jumla ya klabu 20 za Ligi Kuu England (EPL) ...

foto
Mwandishi: Stella Nyemenohi

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi