loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

'Nilikiona kifo, dawa ya NIMR imeniponya'

WAGONJWA walioponeshwa na dawa ya Nimrcaf inatengenezwa na Taasisi ya Utafi ti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR) wametoa ushuhuda mkubwa namna dawa hiyo ilivyowasaidia hadi kurudia hali zao za kawaida baada ya kupata homa kali ya mapafu inayosababishwa na virusi vya corona (Covid-19).

HabariLEO imezungumza na wagonjwa watatu waliopona kutokana na kutumia dawa hiyo ambayo imeonesha mafanikio makubwa na sasa watu wengi wanaisaka ili kutibu virusi hivyo ambavyo vimesababisha vifo vya watu zaidi ya 300,000 duniani kote na zaidi ya milioni tatu kuambukizwa.

Akisimulia alivyoanza kuumwa, mkazi wa jijini Dar es Salaam, Lulu Mohamed alisema, “nilianza kujisikia vibaya siku ya Jumatano wiki ambayo Jumamosi yake ndio tulikuwa tunaanza kufunga mwezi wa Ramadhani… kwanza nilianza kupoteza uwezo wa kusikia harufu na kupoteza uwezo wa kusikia ladha ya chakula, nikawa anajisikia ovyo, nameza Panadol na kuendelea na shughuli zangu.”

Lulu aliongeza: “Alhamisi hali ikawa ile ile, nikawa nameza tu na pakiti yangu nzima ya panadol kila baada ya muda nameza naendelea na shughuli zangu…Ijumaa hali ikawa mbaya, lakini ikawa bado najisikilizia, Jumamosi tunaanza kufunga nikafunga, Jumapili pia nilifunga.

“Jumatatu hali ikawa mbaya zaidi kupumua siwezi, mimi nina pumu nikadhani ni pumu, watoto wakampigia dada yangu akaja na kunipeleka hospitali,” alibainisha na kuongeza kuwa hospitali alichomwa sindano ya pumu na kutakiwa kurejea nyumbani ambako alijiweka karantini, kutumia dawa alizopewa hospitali na kujifukiza.

Hata hivyo, alisema hali ilikuwa mbaya zaidi Jumanne na kurudishwa tena hospitalini ambako aliwekewa dripu.

“Sikufichi nilikuwa naumwa sana kichwa, mwili haukuwa na nguvu ni kama nilianza kupararaizi mkono wa kushoto na mguu wa kushoto, hospitali walinichoma choma sindano na kukamua damu lakini ilikuwa haitoki, ilikuwa imeganda, nilikata tamaa, nilikiona kifo, hata wanangu walishakata tamaa,” alieleza.

“Fikiria hali yote hiyo imenitokea na nilikuwa najifukiza na natumia ‘inhelar’… nimechomwa sindano achilia mbali madawa lakini haikusaidia.

“Namshukuru Mungu sana kwa kuwaongoza NIMR kutoa hii dawa imenisaidia, nililetewa chupa moja nikatakiwa ninywe vijiko viwili, lakini mimi nilimimina kwenye kikombe kimoja cha kahawa na kuinywa yote,” alisema Lulu ambaye alikuwa akijiuguzia nyumbani.

“Unajua maumivu niliyokuwa nayapata nilijikuta nakunywa dawa bila mpangilio ndio maana walikuwa wanaficha, hata hii ya NIMR baada ya kuona nimekunywa kikombe cha kahawa badala ya vijiko viwili waliificha,” alisimulia.

Akiendelea kutoa ushuhuda wa dawa hiyo, alisema baada ya kunywa dawa hiyo ikiwa ni majira ya saa moja usiku, alianza kuona mabadiliko katika mwili wake ndani ya nusu saa.

“Zilipita kama dakika 30 hivi nikasikia joto la ajabu katika mwili, tukasema labda shauri ya pilipili iliyopo, lakini baadaye pua zikafunguka, zilikuwa zimeziba zikafunguka, kwenye saa tano usiku watoto walipoenda kulala nikanyata, hadi sebuleni nikaiiba na kuinywa tena ujazo wa kikombe cha kahawa ambacho kinaingia vijiko vinne,” alieleza Lulu.

Alisema alilala usingizi mzuri siku hiyo ambapo alishtuka saa 12 alfajiri akiwa na njaa kali ya ajabu ambayo ulimpelekea kuanza kutetemeka.

“Niliwaamsha wakanipa chai, nikanywa tena dawa nikapata nguvu ambazo awali sikuwa nazo, niliweza kufanya mazoezi na mchana nikanywa tena…mimi ni shahidi wa hii dawa, nitasimama popote kuisemea bila woga, imenisaidia sana.

“Naamini hii dawa ya NIMR ni bora kuliko hata hiyo ya Madagascar, hali niliyokuwa nayo mwanzo eti sasa hivi naweza kutembea, siamini, namshukuru Mungu, dawa hii ni kiboko mtu akitumia akafa basi ni kwa rehema za Mungu,” alieleza.

Aliongeza: “Nimepona ila kwa sasa bado natumia na familia yangu kama kinga kwa utaratibu na tunaendelea kujifukiza ili ugonjwa usirudi tena.”

Mkazi wa jijini Dodoma akitoa ushuhuda wa dawa hiyo alisema, “nilikuwa naumwa sana kichwa, mwili unauma, mgongo hata kukaa nilikuwa siwezi, visigino kukanyaga chini nilikuwa siwezi, nilikua natapika sana hakuna kitu kilikuwa kinakaa mdomoni.”

Aliongeza, “nikakumbuka dada Lulu alitoa ushuhuda wa hii dawa ya Nimrcaf kwenye group ndio nikamuliza Lulu mi nitaipataje nahisi hali kama yake, nashukuru Farida (mmoja wa wanakikundi) akasema amezinunua, akanitumia kwenye basi toka nimeanza kutumia sasa ni mzima, Mungu ambariki sana aliyegundua tiba hii.”

Mhandisi mkazi wa jijini Dar es Salaam pia ametoa ushuhuda, akieleza kuwa alikuwa anasumbuliwa na tatizo la kubanwa mbavu, lakini alipotumia dawa hiyo hali hiyo haisikii tena.

“Nilikuwa siwezi kukaa kwenye AC (kiyoyozi) hata kwenye gari nikiwasha baada ya muda mbavu zinanibana sana, lakini toka nimeanza kuitumia Nimrcaf nimepata matokeo mazuri hali hiyo sisikii tena, hata usingizi nalala vizuri,” alisema mhandisi huyo aliyeomba asitajwe jina gazetini.

Ushuhuda wa watu hao unatoa mwanga wa matumaini zaidi wa dawa hiyo ambayo imefanyiwa kazi na NIMR kwa wagonjwa wa homa kali ya mapafu inayosababishwa na virusi vya corona.

Dawa hiyo iliyopewa jina la NIMRCAF inatokana na mchanganyiko wa vyakula; na katika majaribio imeonesha ina uwezo mkubwa wa kudhibiti virusi vya corona.

Akielezea mchanganyiko huo, Mkurugenzi wa Kitengo cha Tiba Asili cha NIMR, Dk Justine Omolo alisema ni fomula ya tiba lishe ambayo ina mchanganyiko wa pilipili kichaa, tangawizi, limao na kitunguu saumu, na maji.

Alisema dawa hiyo inasaidia kumpa nafuu mgonjwa wa corona, kwa kutibu dalili zinazotokana na ugonjwa huo. Kwamba tayari imeshaonyesha matokeo chanya.

“Mchanganyiko wa tiba lishe hiyo sio dawa ya corona, lakini inasaidia kumpa nafuu mgonjwa wa corona kwa kuwa inatibu dalili zinazoambatana na ugonjwa huo,” alisema.

Alisema mpaka sasa tiba lishe hiyo imeshaleta matokeo chanya kwa kuwa imesaidia wagonjwa wengi wa corona. Alisema kwa sasa mahitaji yamekuwa ni mengi, tofauti na awali.

Kwa mujibu wa Dk Omolo, NIMRCAF ina vitamini C kwa wingi na vitamini K, na kitaalamu mchanganyiko unaopatikana katika tiba lishe hiyo unaitwa ‘Polyphenols’. Mchanganyiko huo unazuia damu kuganda.

Alisema seli zinazopokea virusi vya corona, zipo kwenye mapafu na virusi vikiingia humo, husababisha damu kuganda na kuleta matatizo kwenye mfumo wa upumuaji. “Mgonjwa akitumia tiba lishe hii, ndani ya nusu saa lazima atasikia nafuu,” alifafanua.

MGOMBEA Urais wa Chama ...

foto
Mwandishi: Vicky Kimaro

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi