loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Kwanini marais Afrika wamefeli kwenye lockdown?

Tumeona kuwa, kufunga uchumi ilikuwa kazi rahisi sana. Lakini, kufungua shughuli za kiuchumi kunawawesesha baadhi ya marais wa Afrika. Nilipata kuandika makala ya mtandaoni alipofeli Cyril Ramaphosa, ilihusu Lockdown.

Nilisema kuwa, alifeli kwenye kuwaambia masikini wake wabaki majumbani wakati hawana hata hizo nyumba zenyewe. Na kwamba, kwa wengine wana vyumba tu vya kujisitiri, lakini hakika ya kula yao ni lazima watoke kwenda kuhemea.

Kwamba viongozi wengi Afrika, kwa kuwaiga wakubwa, wamejikuta wakiingia kwenye mtego wa kuzifunga nchi zao (Lockdown) bila kuwa na mipango thabiti ya namna ya watakavyowasaidia raia wao wengi wenye hali duni.

Wahenga walisema; Usimuige tembo kwa kila kitu. Leo Rais Cyril Ramaphosa amekiri hadharani kuwa, lockdown iliwatesa wanyonge. Na kwa vile kuna wengi wamekasirishwa, Ramaphosa nae anapata tabu kwenye kufungua.

Mei Mosi alitangaza itakuwa siku ya kuanza kufungua. Ilivyo Afrika, Rais anaweza kwa urahisi kufunga uchumi, lakini unapofungua lazima uwe na maelezo pia kwanini ulifunga na huku unafungua tatizo likiwa bado lipo? Ikumbukwe, Afrika Kusini ina watu 200, 000 wasio na makazi. Wengi wao wako Johannesburg.

Kufunga nchi kwa maana ya kusimamisha shughuli za kiuchumi ni moja ya hatua za kukabiliana na kuenea kwa maambukizi ya corona.

Hata hivyo, hatua hiyo inataka umakini mkubwa. Kuna nchi zimeharakisha kwenda kwenye hatua hiyo na kusababisha athari zaidi kwa watu wake.

Nikaweka bayana kuwa, modeli ya Tanzania bado inafanya kazi na hadi sasa imeepusha athari zaidi za kiuchumi na kijamii.

Rais Magufuli alikuwa na ujasiri wa kiuongozi kuliona tatizo la ku- lockdown na kuvumilia shutuma zote.

Inachohitaji Tanzania baada ya kudhibiti viwanja vya ndege, ni kudhibiti mipaka ya nchi kavu na majini na huku ikiongeza elimu ya umma juu ya kujikinga na janga hilo.

Kwa nini Afrika inawaumiza vichwa watafiti wa Dunia? Tumeona kuwa, wakati corona imetikisa Ulaya na Amerika, Afrika kama bara limeonekana kutopata dhoruba kubwa.

Idadi ya vifo vilivyoripitiwa rasmi hadi sasa barani Afrika havizidi idadi ya vifo katika nchi moja ya Ulaya, Sweden. Afrika imeripoti vifo 1,911, wakati Sweden imeripoti vifo 3,000. Kati ya mataifa 54 ya Afrika, taifa la Lesotho halijaripoti hata kisa kimoja. Kulikoni? Swali hili linawaumiza vichwa watafiti duniani. Kuna majibu.

Watalaamu wanasema kuwa, Afrika inaendelea kuhimili corona kutokana na yafuatayo; Afrika ni bara ambalo kwa historia, lina uzoefu wa kukabiliana na majanga ya kiafya na kuwa watu wake wamepitia majanga makubwa ya kiafya kama vile ebola, homa ya bonde la ufa na hata kimeta. Idadi kubwa ya watu wa Afrika ni vijana.

Ni asilimia tatu tu ya watu wote wa Afrika wenye umri unaoanzia miaka 65. Kundi hilo la wazee ndilo lililo katika hatari kubwa ya kuathiriwa vibaya na corona.

Hata hivyo, corona inaweza kuwa na madhara makubwa Afrika kwa vile bara la Afrika lina idadi kubwa ya watu wenye kuathirika na magonjwa mengine kama vile ukimwi , kisukari na kifua kikuu.

Wenye magonjwa haya na mengine wamo pia kwenye hatari ya kuathirika vibaya na corona. Kwenye kundi hili kuna vijana wengi wa Afrika.

Na kubwa zaidi, corona inaweza pia kumuua hata kijana asiye na ukimwi wala kifua kikuu, wanasema wataalam.

Na Lockdown je?

Imedhihirisha kuwa, lockdown imekuwa na madhara zaidi kwa Waafrika kuliko corona yenyewe. Watu wengi wameteseka na njaa na wataendelea kuteseka na njaa na hata wengine kufa kwa njaa wakati na hata baada ya corona.

Ajabu ya Waafrika kuiga ya Ulaya! Kuna viongozi wa nchi za Afrika walikurupuka kuweka lockdown na kusahau kuwa, Afrika imeshawahi kuwa na majanga yake na haijawahi kuwa na lockdown.

Ebola ni mfano mmoja, kati ya mwaka 2014- 2015 nchi za Afrika Magharibi zilikabiliwa na janga la kutisha la ebola. Dunia pia iliingia hofu kubwa.

Hata nchi jirani na Tanzania ya Kongo- Kinshasa ilikuwa kwenye hali mbaya.

Hata hivyo, hakukuwa na lockdown Kinshasa wala Monrovia. Na wala Tanzania kama nchi hatukufunga mipaka yetu na Kongo- Kinshasa. Iweje Afrika leo iingiwe na taharuki ya kufunga shughuli za kiuchumi? Naam, tujihadhari, tusitaharuki.

KATIKA jumla ya klabu 20 za Ligi Kuu England (EPL) ...

foto
Mwandishi: Maggid Mjengwa

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi