loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Pongezi nchi EAC kuokoa uchumi

NCHI za mbalimbali duniani zimeanza kulegeza masharti ya amri ya kutotoka nje ikiwa ni njia mojawapo ya kukabiliana na janga la virusi vya corona (COVID-19).

Nchi hizo sasa zimeruhusu biashara kadhaa kufunguliwa, shule kujerea huku wakichukua tahadhari kutokana na ukweli kwamba maisha na uchumi lazima yaendelee licha la uwepo wa ugonjwa huo.

Hatua hiyo, imekuja ikiwa ni zaidi ya mwezi sasa tangu mataifa kadhaa duniani yaweke amri ya kufunga mipaka yake, kutotoka nje huku pia kazi zikisimama na shule kufungwa ili kupambana na corona.

Hata hivyo, Tanzania kwa upande wake, haikuweka kabisa zuio kama hilo kwa kutambua kuwa hatua hiyo inaweza kusababisha athari kubwa zaidi kuliko hata corona yenyewe.

Badala yake, Tanzania iliwataka wananchi wake kuchukua tahadhari kwa kufuata maelekezo ya wataalamu wa afya na serikali kuhusu njia za kujikinga na ugonjwa huo.

Akisisitiza hilo, Rais Dk John Magufuli katika hotuba yake ya Aprili 22, mwaka huu, alisema kuwa hatafunga jiji lolote ikiwemo Jiji la Kibiashara la Dar es Salaam ili kuwezesha shughuli za kiuchumi kuendelea kama kawaida ili kulijenga taifa letu.

Nchini Afrika Kusini, ambayo iliwekwa amri kwa raia wake kutotoka nje, wameanza kulegeza ambapo kuanzia Mei Mosi, mwaka huu baadhi ya huduma na biashara zimefunguliwa huku wakisisitiza watu kuchukua tahadhari.

Aidha, nchi hiyo imeruhusu wananchi kutoka majumbani kwa muda kidogo na kwenda kufanya mazoezi kwa muda wa saa tatu kisha kurudi nyumbani lakini amri ya kutotembea usiku bado iko pale pale.

Rwanda, Kenya na Uganda ni nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki ambazo ziliweka amri ya kutotoka nje lakini raia wake wanakabiliwa na hali ngumu ya maisha, hatua ambayo imeanza kusababisha ghasia na vurugu za hapa na pale.

Rwanda kwa upande wake, sasa wamelegeza masharti hayo na kuanzia Jumatatu iliyopita baadhi ya maeneo ya kazi yalifunguliwa ikiwa ni njia ya kukuza uchumi wao usiendelee kushuka.

Tunachukua fursa hii kuyaasa mataifa ya Afrika Mashariki kuendelea kuchukua tahadhari dhidi ya maambukizi ya corona kwa wananchi wake lakini bila kukubali kuacha uchumi wa mataifa hayo kushuka kwani janga litakalotokana na kudorora kwa uchumi kwa nchi za Afrika Mashariki litakuwa kubwa zaidi.

Tunasema hivyo kutokana na kuwa na mifano hai kutoka katika mataifa yaliyoendelea ikiwa Marekani ambayo pamoja na kuwa na uchumi imara lakini amri hiyo ya kuzuia watu kutoka nje imeanza kuleta madhara makubwa hatua ambayo imelifanya Taifa hilo kuingia katika vurugu kwa wananchi kuandamana mitaani wakishinikiza kuruhusiwa kuendelea na shughuli za kiuchumi.

WIKI hii kumekuwa na taarifa za Yanga kutakiwa ...

foto
Mwandishi: Mhariri

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi