loader
Picha

Corona yaingia Ikulu Marekani

WAFANYAKAZI wa Ikulu nchini Marekani wameagizwa kuhakikisha kuanzia sasa wanavaa barakoa wanapoingia jengo la West Wing, baada ya wafanyakazi wawili kukutwa na maambukizi ya virusi vya corona.

Ofisi ya wafanyakazi wa Ikulu hiyo ilisema jana ni lazima kila mfanyakazi afunike uso wake isipokuwa tu pale watakapokuwa wamekaa kwenye meza zao na kufanya kazi huku kila mmoja akitakiwa kukaa umbali wa mita moja.

Agizo hilo limetolewa baada ya Msaidizi wa Makamu wa Rais wa Marekani, Mike Pence pamoja na mfanyakazi wa ndani binafsi wa Rais wa Marekani, Donald Trump kukutwa na maambukizi ya virusi hivyo.

Hata hivyo, Rais Trump alieleza inahitajika kuwa na sera kuhusu agizo hilo. Alipojitokeza mbele ya waandishi wa habari bila kuvaa barakoa jana, rais huyo alisema haina haja ya yeye kutii agizo hilo la kuvaa barakoa kwa kuwa anajiweka mbali na watu wengine.

“Kuna mamia ya watu wanaingia na kutoka Ikulu kila siku, nafikiri mpaka sasa tunafanya vizuri katika kuudhibiti ugonjwa huu,” alisema Trump.

Wajumbe watatu wa kikosi kazi cha Ikulu dhidi ya virusi vya corona, walijiweka karantini kwa muda wa wiki mbili baada ya kubaini kuwa na ukaribu na watu walio na maambukizi ya virusi hivyo. Wajumbe hao ni Dk Anthony Fauci, ambaye amekuwa mstari wa mbele katika mapambano dhidi ya virusi hivyo nchini humo.

Katibu Muhtasi wa Makamu wa Rais, Pence, Katie Mller ambaye ni mke wa Msaidizi wa Rais Trump, Stephen Miller amekutwa na maambukizi ya corona. Vipimo vyake vilikuja baada ya mfanyakazi wa ndani binafsi wa Rais Trump naye kukutwa na maambukizi na kuanza kuugua.

Hata hivyo, kiongozi huyo alibainisha kuwa maambukizi hayo si ya kutisha kama inavyodhaniwa kwa sababu wote walio na maambukizi wamekutana na mtu mmoja tu ambaye naye amepima na kukutwa hana maambukizi.

Mpaka sasa Marekani ndio nchi inayoongoza kwa maambukizi na vifo vinavyotokana na virusi vinavyosababisha ugonjwa wa covid 19. Nchi hiyo ina watu waliopata maambukizi milioni 1.385 na vifo 81,795.

SERIKALI nchini Canada imeidhinisha kufanyika kwa majaribio ya kwanza ya ...

foto
Mwandishi: WASHINGTON, Marekani

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi