loader
Picha

‘Habari za wanaodaiwa kufa kwa corona Moro ni za uongo’

SERIKALI imekanusha taarifa zilizotolewa na baadhi ya mitandao ya kijamii zinazosema watu 92 wamekufa mkoani hapa kwa corona katika kipindi cha wiki moja iliyopita na kuzikwa makaburi ya Kola, Manispaa ya Morogoro.

Hayo yalibainishwa na Mganga Mkuu wa Serikali, Profesa Abel Makubi mjini hapa baada ya kutembelea eneo hilo la makaburi na kufanya uchunguzi wa kuyaona makaburi hayo kama yanavyotangazwa.

“Kumekuwepo na taarifa zinazoashiria matumizi yasiyo sahihi ya kimtandao na hivyo kuleta taharuki kwa wakazi wa Morogoro imefika hapa nijionee mwenyewe makaburi hayo 92, sijayaona hayo makaburi yaliyosemwa,” alisema Profesa Makubi.

Katika ziara hiyo, Profesa Makubi alitembelea sehemu zote za makaburi hapo Kola ikiwa pia kupata taarifa kutoka kwa vijana wachimba makaburi ambao wamekuwepo hapo zaidi ya mwaka.

Aidha, Mganga Mkuu wa Serikali aliwaasa baadhi ya wananchi kuacha kupotosha jamii kwa taarifa za uongo kama kwamba wao wanafurahia vifo. Naye Mtunzaji wa makaburi hayo, Ally Kasole ambaye alihojiwa pia alisema maneno hayo ni uvumi maana hajawahi kuona kuchimbwa makaburi ya idadi hiyo kwa kipindi hicho.

Alisema ni makaburi sita tu (kwa sababu mbalimbali za vifo) kwa siku tano zilizopita na hakuna maziko ya usiku yanayofanyika kwenye makaburi hayo ya Kola. Kauli hiyo ilisisitizwa pia na wachimbaji wegine wa makaburi ambao walikutwa hapo.

Profesa Makubi amewatahadharisha ndugu wa marehemu kuacha kufungua miili ya marehemu iliyokwisha kufungwa na wataalamu wa afya. Vilevile amewataka wananchi kuendelea kujikinga na ugonjwa huo, kwa kuacha misongamano, kuvaa barakoa pamoja na kuzingatia usafi wa kunawa mikono kwa maji yanayotiririka na sabani.

Pia aliwasisitiza watumishi wa Afya kuendelea kusimamia uandaji wa maziko ya marehemu wote kwa kufuata utu na heshima ya binadamu kwa kushirikisha familia kwa karibu.

AWAMU ya Kwanza ya Serikali ya Tanzania iliyoongozwa na Mwalimu ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Maalumu, Morogoro

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi