loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Wachezaji wajisalimisha polisi

WACHEZAJI wa NFL, Deandre Baker na Quinton Dunbar, walimejisalimisha kwa polisi baada ya kushtakiwa kwa wizi wa kutumia silaha huko Florida, Marekani. Mlinzi wa pembeni wa New York Giants, Baker, mwenye umri wa miaka 22, ambaye anashutumiwa kwa kushambulia, alijisalimisha Jumamosi asubuhi, wakili wake alisema.

Dunbar mwenye umri wa miaka 27, anayechezea Seattle Seahawks, baadaye pia alijipeleka polisi. Wachezaji hao wanatuhumiwa kwa kuwaibia wageni wakiwa na bunduki kwenye sherehe wiki iliyopita.

Karibu dola za Marekani 12,000 taslimu na saa ambazo thamani yake ni hadidola 25,000 inaaminika zilichukuliwa katika mji wa Miramar, Jumatano. Mawakili wa utetezi wa wachezaji wote walisema mashuhuda walikuwa wametia saini hati ya kumbukumbu kwamba wachezaji hao hawakuhusika katika wizi huo.

Kwa mujibu wa kibali cha polisi cha kukamatwa, tukio hilo lilitokea baada ya mabishano kuzuka kwenye sherehe, ambapo wageni walikuwa wakicheza karata na michezo ya kubahatisha.

Baker inadaiwa alitoa bunduki kabla ya Dunbar na mtu mwingine aliyetajwa kuwa alivaa kofia nyekundu kuanza kuchukua vitu vya thamani na fedha kutoka kwa watu. Mtu aliyekuwa amevaa barakoa nyekundu hajatambuliwa katika ripoti. Baker inadaiwa alimwuliza mtu aliyepiga risasi ambaye ni shahidi, lakini mtu aliyevaa barakoa nyekundu hakufanya hivyo.

Hati ya mashitaka ya polisi ilisema shahidi mmoja alikuwa chini ya shinikizo na kuwa hilo lilipangwa kwa kuwa magari yote matatu yalitoweka haraka eneo hilo.

Baker anakabiliwa na mashtaka nane, manne ya wizi wa kutumia silaha na manne ya kushambuliwa kwa silaha ya moto. Dunbar ameshtakiwa kwa makosa manne ya wizi wa kutumia silaha.

NFL inasema inajua tukio hilo, lakini haijatoa maoni. Taarifa iliyotolewa na New York Giants ilisema walikuwa wamewasiliana na Deandre Baker na hawakuwa na maoni yoyote. Seattle Seahawks walisema wamesikia tukio hilo na bado wanakusanya taarifa.

foto
Mwandishi: FLORIDA, Marekani

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi