loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

EAC ishikamane kukabili corona

JANGA la maambukizi ya virusi vya ugonjwa wa homa ya mapafu, Covid 19 unaotokana na virusi vya corona halijaziacha salama nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) na Afrika kwa ujumla.

Karibu zote zina visa vya maambukizi. Kutokana na nchi hizo kuwa na kiwango tofauti cha maambukizi, kila moja imekuwa ikichukua njia zake za kupambana dhidi ya virusi hivyo.

Mfano, Tanzania imekataa kufungia ndani watu wake ikiwaacha waendelee na kazi za uzalishaji mali, kutofunga mipaka na majirani ili wasiathirike.

Lakini nchi nyingine za EAC zimefungia watu wake ndani zikiwapa fedha, vyakula na mahitaji mengine.

Zimefanya hivyo kwa kutumia raslimali zake huku nyingine zikiwa zimekopeshwa fedha na Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) kusaidia.

Hata hivyo, pamoja na watu kupewa fedha, ziko dalili za raia wa baadhi ya nchi kutokubaliana na kufungiwa na kuanza kulazimisha kuachiwa.

Wanaolilia kuachwa huru wanadai kuchoka kukaa nyumbani bila kazi kwa miezi mitatu tangu corona izuke huku hawajui hatma yake.

Tunaungana na Watanzania kuwapa pole ndugu zetu EAC na Afrika kwa ujumla kwa pigo hili linalotishia uchumi, usalama wa chakula, uhusiano wa diplomasia.

Tunaipongeza Serikali ya Tanzania kusimama imara na kuacha raia wake kuendelea kuzalisha mali na kutowafungia majirani mipaka yake na pia kuendeleza uhusiano mzuri wa kidiplomasia.

Wakati tukimpongeza Rais Dk John Magufuli kwa hilo, tumesikitishwa na mwelekeo wa nchi nyingine Afrika kusahau umuhimu wa umoja.

Ni kweli dunia ina taharuki ya corona lakini hatua za kuikabili hazitakiwi kuzigawa nchi za Afrika bali zinatakiwa kuungana ili kuikabili.

Ni katika umoja wenye nguvu Afrika na nchi nyingine duniani zitaweza kukabili Covid 19 na kuishinda hivyo zifanye maamuzi zikizingatia kuwa umoja ni nguvu na utengano ni udhaifu.

Kama alivyosema Rais Magufuli Tanzania ni nchi huru, haiwezi kupangiwa cha kufanya hivyo tunaheshimu uhuru wa nchi za Afrika kuamua njia zinazowafaa kukabili ugonjwa huo.

Hata hivyo, kwa kurejea malengo ya umajumui wa Afrika, tunawiwa kutoa angalizo nchi za Afrika kutosahau utangamano wao wa kikanda.

Utangamano wa kikanda wa EAC, ECOWAS na SADC, IGAD umelenga kuzipa nchi za Afrika, sauti dhidi ya nchi zilizoendelea duniani.

Yote hii ni katika kuhakikisha ustawi wa mtu mweusi kwanza hivyo nchi zikumbuke hilo. Hatua za kukabili corona huku zikionesha dalili ya kuathiri uhusiano wa kidiplomasia na nchi nyingine hazipaswi kuachwa tu ziendelee.

FUKUTO la Uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani linazidi ...

foto
Mwandishi: Mhariri

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi