loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Wakala wa Majengo wamkera Waziri

WAZIRI wa Nchi, Ofi si ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Seleman Jafo ameitaka Halmashauri ya Chalinze wilayani Bagamoyo Mkoa wa Pwani, kutafuta mkandarasi mwingine wa jengo jipya la halmashauri hiyo baada ya Wakala wa Majengo (TBA) kushindwa kukamilisha ujenzi kwa wakati.

Aidha, amewataka TBA kukamilisha awamu ya kwanza ya ujenzi ifikapo Mei 30, mwaka huu na kazi hiyo apewe mkandarasi mwingine ili akamilishe kazi hiyo ili huduma kwa wananchi zianze kutolewa.

Aliyasema hayo jana alipotembelea kukagua ujenzi wa jengo hilo la halmashauri unaofanywa Bwilingu ambalo ujenzi wake ulianza tangu mwaka 2018 na kutakiwa kukamilika mwaka huo huo, lakini hadi sasa halijakamilika ambalo mara litakapokamilika litagharimu kiasi cha Sh bilioni 5.7.

“Sijaridhika niliuliza kama tatizo ni fedha mkasema kuwa fedha zipo lakini kazi haikamiliki hamfanani na TBA kule Dodoma, majengo kama haya yamekamilika na kwa gharama ndogo na nyie mnatumia fedha nyingi, lakini mnakwenda taratibu. Hakikisheni Mei 30 hatua ya kwanza inakamilika baada ya awamu ya kwanza kukamilika TBA msifanye kazi hii tena. Hatuwezi kusubiria miaka miwili baadhi ya kazi hazifanyiki leo mmekuja zimamoto mkimaliza hapo halmashauri tafuteni mkandarasi mwingine ili akamilishe hatua zilizobakia,” aliagiza Jafo.

Alisema haiwezekani kufanya kazi kwa utaratibu kama huo mkurugenzi na timu yake wafanye utaratibu wa kukamilisha kazi TBA hawataweza kukamilisha baadhi ya maeneo wamefanya kazi vizuri, lakini Chalinze wameshindwa kama wangekuwa makini kazi hiyo ingekuwa imeisha.

Meneja wa TBA Mkoa, Asha Myanza alisema kulikuwa na changamoto kubwa ikiwa ni pamoja na udongo wa eneo hilo na upatikanaji wa maji.

BEKI  wa zamani wa ...

foto
Mwandishi: John Gagarini, Chalinze

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi