loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

'Wanahabari jifunzeni jinsia, uchaguzi'

MWENYEKITI wa Mtandao wa Wanawake na Katiba, Uchaguzi na Uongozi (WFT) Profesa Ruth Meena amesema wanahabari wanapaswa kujielimisha masuala ya jinsia katika mchakato wa uchaguzi kubaini mapengo ya utekelezwaji wa sheria za uchaguzi kwa mlengo wa jinsia.

Amesema hayo kwa video akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na mtandao huo kufanyia uchambuzi sheria tano za uchaguzi.

Alisema maarifa hayo yatawapa wanahabari nyenzo ya kutetea haki ya ushiriki wa wanawake katika mchakato wa uchaguzi.

“Ninyi wanahabari ni wadau muhimu katika utetezi wa haki za wanawake, mna nafasi kubwa ya kuleta mabadiliko tunaamini mtakapopata maarifa mtatumia kama nyenzo ya kutetea haki za wanawake katika uchaguzi na uongozi na mtumie takwimu kama nyenzo za kutetea ushiriki wa wanawake katika uchaguzi,”alisema.

Pia Profesa Meena alisema malengo mahususi ya uchambuzi huo ni kutoa muhtasari mambo yaliyojitokeza kwenye baadhi ya sheria za uchaguzi ili kubainisha mapengo yanayoweza kuwa kikwazo katika kutekeleza azma ya ujenzi wa demokrasia shirikishi kwa mlengo wa jinsia .

Alisema sheria hizo ni Sheria ya Taifa ya Uchaguzi Sura ya 343 ya 2015, Sheria ya Uchaguzi ya Zanzibar namba 4 (2018), Sheria ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa namba 4 ya mwaka 1979 namba 292 kama ilivofanyiwa marekebisho mwaka 2010 na mwaka 2015).

Pia Sheria ya Serikali Za Mitaa (Mamlaka za Wilaya Sura 287 kama ilivyorekebishwa 2002) na Sheria za Serikali za Mitaa za mmlaka za miji sura ya 288 na mamlaka za wilaya sura ya 287.

Mkutano huo ulilenga kuwezesha wanahabari kupata taarifa za kina zenye uchambuzi wa sheria zilizochambuliwa kwa mlengo wa jinsia kwani wanahabari ni muhimu kwenye ujenzi wa demokrasia shirikishi na kwenye harakati za ukombozi wa wanawake

BEKI  wa zamani wa ...

foto
Mwandishi: Sifa Lubasi, Dodoma

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi