loader
Picha

Elimu muhimu kudhibiti fistula

KILA mwaka Mei 23, dunia huadhimisha siku ya kutokomeza fi stula ambapo elimu sahihi kuhusu tatizo hilo inatakiwa kutolewa kwa kina.

Elimu hiyo ni muhimu ili wale watakaoathirika waweze kuchukua hatua haraka na kupatiwa matibabu kwa kuwa ugonjwa huo hupona.

Fistula husababisha shimo kubwa kati ya njia ya uzazi na njia ya mkojo unatokana na mama kuwa na uchungu wa muda mrefu bila tiba.

Nchini Tanzania, ugonjwa huo umeendelea kusumbua kina mama wengi ingawa wapo waliojitokeza na kupatiwa matibabu na kupona, wengine wakijificha kwa aibu wakiendelea kunyanyapaliwa na hata kutengwa na jamii.

Katika kuhakikisha ugonjwa huo unatokomeza nchini, Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto kwa kushirikiana na Mashirika ya Umoja wa Mataifa yamejikita kutoa elimu kwa wingi kwa jamii muathirika anavyoweza kujitokeza na kupatiwa matibabu yanayowezesha hali yake kurudi kama awali na kuendelea na majukumu yake kama kawaida.

Wasichana na wanawake walioathirika na ugonjwa huo unaozuilika kwa kiasi kikubwa huwa wanakosa huduma, matokeo yake wanakumbana unyanyapaa katika jamii.

Kukosa kwao matibabu ya haraka kunadhoofisha afya zao na utu wao na ni ukiukwaji wa haki zao za binadamu na hutengewa kwa kuonekana hawastahili kuendelea kujumuika katika jamii.

Ikumbukwe suala la unyanyapaa ni ugonjwa mbaya zaidi kwa mgonjwa kwa kuwa iwapo alikuwa na uwezo wa kufanya shughuli zake za kuingiza kipato, hawezi tena akihofia kuwa kila anayekutana naye atakuwa anamnyanyapaa.

Vilevile wapo wanaopatwa ugonjwa huo na kujikuta katika wakati mgumu kimaisha, wakichekwa wakishindwa hata kuhudhurua shughuli za kijamii, kushiriki shughuli za ibada huku jamii ikiwatenga kwa sababu ya hali hiyo.

Si kila anayepata ugonjwa huo hupanga, la hasha wakati mwingine wasichana, wanawake ambao hukabiliana na tatizo hilo, hufuata masharti yote wakati wa ujauzito na bado bahati mbaya huwakuta wakati wa kujifungua.

Aidha, wapo waathirika ambao waliweza kuhudhuria kliniki punde tu walipojitambua wana ujauzito na hadi miezi yote tisa lakini wakati wa kujifungua mambo yalibadilika na kuwa mabaya wakipata fistula ya majeraha.

Pia wapo wanaume wanaowaacha wake zaowanapobainika na fistula, jambo ambalo kwa mtizamo mwingine husababisha unyanyapaa katika jamii na utu wa mwanamke kutwezwa.

Kwa mujibu wa Shirika la Kimataifa la Idadi ya watu Duniani (UNFPA) inakadiriwa wanawake milioni mbili Kusini mwa Jangwa la Sahara, Asia, ulimwengu wa Kiarabu, Amerika Kusini na Caribbean wanaishi na fistula na visa vipya kati 50,000 hadi 100,000 hutokea kila mwaka.

Maadhimisho hayo ni fursa jamii kuelimisha wanawake wenye tatizo hilo wakitambua Kituo cha huduma ya afya ya Jamii (CCBRT) hutoa huduma bure kwa waathirika. Pia fursa wanawake kupata elimu sahihi kuhusu fistula na wanapopatwa na tatizo kuwaokoa wengi na wale wanaonyanyapaliwa kupona.

KUIBUKA kwa ugonjwa wa COVID-19 katika nchi mbalimbali duniani kumesababisha ...

foto
Mwandishi: Lucy Lyatuu

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi