loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Makumbusho Kalenga kuboreshwa

WIZARA ya Maliasili na Utalii imepanga kuboresha miundombinu ya Kituo cha Makumbusho ya Kalenga ili kukidhi mahitaji ya watalii. Hayo yalielezwa bungeni jana kwenye majibu yaliyotolewa na wizara hiyo wakati wa kujibu swali la msingi la Mbunge wa Viti Maalumu, Zainabu Mwamwindi (CCM).

Mwamwindi alitaka kujua mkakati wa serikali wa kuboresha miundombinu ya Kituo cha Kalenga chenye kumbukumbu nyingi za Chifu Mkwawa ili kuvutia utalii.

Majibu ya wizara kwa swali hilo yalifafanua kuwa Makumbusho ya Kalenga ni kielelezo cha makazi ya jadi ya Chifu Mkwawa na Wahehe na katika makumbusho hii kumehifadhiwa fuvu la Chifu Mkwawa lililorudishwa kutoka nchini Ujerumani Julai 9, 1951.

Kutokana na umuhimu wa kituo hiki, Wizara kwa kushirikiana na Halmashauri ya Wilaya ya Iringa imepima mipaka ya Kituo mwaka 2018/2019 na viwanja viwili Na 41 chenye ukubwa wa ekari 6.5 na 42 chenye ekari 1.1 ambavyo vimeingizwa kwenye ramani Na. 100574 ya eneo la kituo cha Kalenga.

“Kwa hivi sasa wizara ipo katika hatua ya mwisho ya kupatiwa hati ya umiliki wa ardhi ya eneo hilo,” ilieleza.

Aidha, wizara imepanga kuboresha miundombinu ya kituo cha Makumbusho ya Kalenga ili kukidhi mahitaji ya watalii, kupitia Mradi wa GEGROW unaotekelezwa kwa ufadhili wa Benki ya Dunia.

Pia wizara imekasimisha jukumu la kuhifadhi na kuendeleza kituo cha Makumbusho ya Kalenga kwa shirika la Hifadhi ya Taifa Tanzania (TANAPA).

Hivyo, kupitia mradi wa REGROW na Tanapa, miundombinu ya Kituo cha Makumbusho ya Kalenga itaboreshwa ikiwa ni pamoja na kujenga kituo cha kumbukumbu na taarifa ili kuhifadhi kumbukumbu ya Mtwa Mkwawa na Utamaduni wa Wahehe, kukarabati majengo yote ya kihistoria yaliyopo katika kituo hicho, na kujenga miundombinu ya huduma za utalii.

Pia wizara itaendelea kusimamia majukumu yote ya uhifadhi, utafiti na kuandaa taarifa zitakazosaidia kuboresha na kutangaza Makumbusho ya Kalenga na kutoa elimu kwa umma juu ya uhifadhi na matumizi endelevu ya malikale.

BEKI  wa zamani wa ...

foto
Mwandishi: Anastazia Anyimike, Dodoma

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi