loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Tanzania yatoa masharti wanaokuja, wanaokwenda

SERIKALI imetoa mwongozo mpya wa wasafi ri wote wa ndani na nje wanaotumia viwanja vya ndege, bahari, reli na barabara huku ikiondoa baadhi ya masharti yakiwemo ya kukaa karantini kwa siku 14.

Mwongozo huo ulitolewa juzi na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu ambaye alisema mwongozo huo mpya wa Mei 18, mwaka huu ni wa tatu ambao unafuta baadhi ya vipengele kwenye mwongozo namba mbili uliotolewa Aprili 2, mwaka huu.

Katika mwongozo huo mpya uliotolewa juzi unalegeza masharti yaliyo kwenye waraka wa pili ambao uliwataka wasafiri wote wanaoingia nchini kukaa karantini kwa siku 14 kama njia mojawapo ya kupambana na maambukizi ya virusi vya corona.

Ummy katika mwongozo huo mpya, alisema wasafiri wote wanaoingia au kutoka lazima wafanye vipimo vya virusi vya corona ili kuhakikisha hawaingizi maambukizi nchini au hawapeleki maambukizi nje.

Aidha, mwongozo huo pia unawataka wasafiri wote kujaza fomu maalumu kuhusu hali ya afya zao na kuonesha mpaka walioingilia au kutokea ili iwe rahisi kutambua na kujua habari zao kwa lengo la kukabiliana na corona.

Pia unawataka wageni wote wanaoingia nchini kuhakikisha wanavaa barakoa na kuzingatia kanuni na maelekezo ya wataalamu wa afya juu ya usafi na kuepuka misongamano.

Kuhusu magari ya mizigo, Waziri Ummy alisema kwa kila gari ya mizigo linatakiwq kuwa na watu wasiozidi watatu ukijumuisha na dereva na kwamba iwapo kuna abiria au rubani, kapteini wa meli au dereva atahisiwa kuwa na maambukizi atawekwa karantini kwenye maeneo yaliyotengwa na serikali.

Kadhalika iwapo dereva aliyebeba mizigo atabainika kuwa na maambukizi mwenye gari atawajibika kutuma dereva mwingine kuja kuchukua gari na kuendelea na safari wakati yule aliyebainika akiwa karantini au hospitali.

Ummy amewataka wananchi wote kuzingatia maelekezo ya wataalamu wa afya na kutoa taarifa kwa kupiga namba 199 kwa huduma za dharura za kiafya.

BEKI  wa zamani wa ...

foto
Mwandishi: Ikunda Erick

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi