loader
Picha

Katwila: TPLB itoe wiki tatu za kujiandaa

KOCHA wa Mtibwa Sugar, Zuberi Katwila amesema kabla ya Ligi Kuu Tanzania Bara kuanza Bodi ya Ligi (TPLB) inatakiwa kutoa muda wa wiki tatu kwa timu kujiandaa.

Katwila ametoa kauli hiyo ikiwa ni siku chache baada ya Rais John Magufuli kusema muda wowote ataruhusu michezo kuendelea endapo hali ya ugonjwa unaosababishwa na virusi vya corona itaendelea kupungua.

Akizungumza kwa njia ya simu jana Katwila, alisema kwa kipindi ambacho michezo ya ligi imesimamishwa kama itatolewa ratiba ya michezo kurejea kitaalamu wanatakiwa kutoa muda wa wiki tatu.

“Muda wa wiki tatu unatosha kwa kocha kuandaa wachezaji ili kuendelea kucheza michezo iliyosalia,” alisema Katwila Katwila ametolea mfano kwenye kikosi chake kwa kipindi ambacho michezo ya ligi imesimama wachezaji wake bado wanaendelea na kufanya mazoezi kulingana na ratiba binafasi aliyopangiwa .

“Licha ya wachezaji kutopata usimamizi lakini wanatambua majukumu yao na wanajua mechi zinarejea ghafla hivyo kwa mchezaji anayetambua majukumu yake atakuwa anafanya mazoezi ipasavyo,” alisema Katwila

Ligi ilisimama Machi 17 baada ya Serikali kutoa tamko la kusimamisha michezo na mikusanyiko kuepusha janga la corona baada ya kuripotiwa kuingia nchini.

SERIKALI baada ya kufanya kikao na wadau wa michezo imesema ...

foto
Mwandishi: Tuzo Mapunda

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi