loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

KMC yatamba kumaliza ligi 10 bora

MSHAMBULIAJI wa KMC, Salim Aiyee amesema wamepanga watakaporejea kwenye ligi wapambane kufa au kupona kuiwezesha timu hiyo kumaliza ligi katika kumi bora.

Aiyee aliyevuma zaidi msimu uliopita akiwa Mwadui FC aliliambia gazeti hili jana kuwa ana imani timu hiyo iliyoanza vibaya ligi itarejea katika kiwango chake na kumaliza ligi kwenye kumi bora.

Alisema anatamani kuona timu hiyo inadumu katika ubora wake ili kubaki na kuanza msimu ujao na nguvu mpya kama ilivyokuwa ule uliopita ilimaliza katika nafasi nne za juu na kuwakilisha nchi kimataifa.

“Ukweli lengo letu tunataka kupambana na kupigana timu imalize ligi ikiwa katika nafasi za kati au juu, nina imani yote yanawezekana kama tutaendelea kucheza kwa umoja tukiwa na lengo moja,” alisema.

Alisema tayari wameanza maandalizi baada ya Rais John Magufuli kutangaza muda wowote michezo kuruhusiwa lakini mashabiki hawataruhusiwa viwanjani kuepusha kuenea kwa virusi vya corona.

Timu hiyo ilianza ligi kwa kusuasua na kujikuta ikiwa katika nafasi za chini kiasi cha kumtimua kocha Jackson Mayanja na kumwajiri Haruna Harerimana na kuanza kuonesha matumaini baada ya kufanya vizuri katika baadhi ya mechi kabla ya ligi kusimamishwa kutokana na virusi vya corona.

Kuhusu mipango yake msimu ujao alisema bado ana mkataba wa mwaka mmoja na nusu na klabu hiyo iwapo kuna timu yoyote itakayomuhitaji ifuate utaratibu kwa kuzungumza na uongozi wake.

Aiyee ni miongoni mwa wachezaji waliofanya vizuri msimu uliopita kiasi cha jina lake kutajwa zaidi na klabu kubwa za Simba, Yanga na Azam lakini akaangukia KMC ambako bado hakuonesha makali yake na alisema kuwa majeruhi kulimrudisha nyuma kidogo.

MWIGIZAJI maarufu wa tamthilia ya Karma, Wema Sepetu amewaomba radhi ...

foto
Mwandishi: Grace Mkojera

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi