loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Tuishi na corona kwa tahadhari

SHIRIKA la Afya Duniani (WHO) hivi karibuni limesema kuwa huenda virusi vya corona, vikaendelea kuwepo na watu kulazimika kuishi navyo, kama ilivyo kwa virusi vya ugonjwa wa Ukimwi, kauli ambayo imewahi kutolewa na Rais Dk John Magufuli.

Kauli hiyo ya WHO ilitokana na hatua ambazo nchi kadhaa duniani, zimenza kuchukua ili kunusuru kuanguka kwa uchumi wake, nchi nyingi zilizokuwa Lockdown sasa zimeanza kusitisha utaratibu huo.

“Virusi hivi vinaweza kuwa ugonjwa mwingine wa mlipuko ambao watu wataishi nao na virusi havitaondoka tena kama ilivyo Ukimwi. Ukimwi haujaondoka lakini tumejua namna ya kuukabili” alisema Mkurugenzi wa Dharura wa WHO hivi karibuni. Itakumbukwa kuwa Mei 3, 2020 Rais Magufuli aliwataka wananchi kuondoa hofu juu ya ugonjwa wa corona, akasema utaondoka kama yalivyoondoka magonjwa mengine.

“Tusitishane, tuchape kazi na kuendelea kuchukua tahadhari. Itakwisha tu au inawezekana tukaishi na huu ugonjwa kama tunavyoishi na Ukimwi” alisema rais Magufuli.

Kufuatia kauli hizo ni kwamba maisha lazima yaendelee, lakini kwa utaratibu maalum, watu kuishi kwa kuchukua taadhari. Tadhari zinazopaswa kuendelea kuchukuliwa ni zile za kuepuka misongamano, kutulia ndani kama huna shuguli ya lazima, kunawa mikono kila mara, ikiwa ni pamoja na kuvaa barakoa.

Watu wasijisahau kwa kuzoea ugonjwa huo, ambao umeshaua zaidi ya watu milioni tatu duniani kote. Kwa sasa hapa nchi, Rais Magufuli amesema mambukizi yamepungua, lakini anasisitiza watu kuchukua tahadhari, kwani ugonjwa bado upo .

Kama ugonjwa bado upo, ni jukumu la kila mmoja kuendelea kuchukua tahadhari za kujilinda ili asiambukizwe, kwani mpaka sasa hakuna uhakika wa kinga au tiba katika siku za kaŕibuni. Ugonjwa huo utaendelea kukua, kama hakutachukuliwa hatua madhubuti kwa mtu mmoja mmoja na kwa pamoja kutokomeza ugonjwa huu sasa.

Nionavyo mimi kabla ya kutoka nyumbani kwako bila barakoa, jiulize unapenda kuumwa? Kama jibu ni hapana, basi utachukua tahadhari ili kujilinda wewe na familia yako, kwa kuvaa barakoa.

Ndiyo maana kuna msemo wa wahenga usemao “Kinga ni Bora kuliko tiba’. Kuna magonjwa fulani hauwezi kuyazuia. Lakini, kuna mambo mengi unaweza kufanya ili kuzuia usipate ugonjwa huu wa corona. Mbali na kuvaa barakoa, watu wasijisahaulishe usafi wa kunawa mikono kila mara kwa maji tiririka na sabuni. Kunawa mikono ni njia moja nzuri ya kuzuia magonjwa au kufanya magonjwa yasiambukize watu wengi.

Tumeona watu wakianza kurudi kwenye utaratibu wao wa kutonawa mikono mara kwa mara na kitendo hicho kuonekana kero kwa baadhi ya watu, Ila nawakumbusha tu kutokunawa ni njia moja nyepesi sana ya kupata mambukizi, kutokana na tabia ya kugusagusa kwenye pua au macho na mikono yenye virusi vya ugonjwa bila kujua. Nionavyo mimi namna nzuri ya kujikinga na ugonjwa huo ni kunawa mikono kila mara.

Kuwa msafi kunaweza pia kuzuia magonjwa hatari sana, kama vile nimonia na kuhara. Kila mwaka magonjwa hayo yanaua watoto zaidi ya milioni mbili ambao wapo chini ya miaka tano. Tabia ya kunawa mikono kila mara, inaweza hata kuzuia ugonjwa hatari sana wa corona usienee haraka. Kuna wakati kunawa mikono, ni jambo la lazima sana ili kulinda afya yako na ya watu wengine.

ZLATKO Krmpotic hadi sasa hajamaliza hata mwezi, tangu amejiunga na ...

foto
Mwandishi: Vicky Kimaro

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi