loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Mfumo wa Kusoma na Kuandika saa kwa Kiswahili

Saa ni neno la Kiswahili lenye asili ya lugha ya Kiarabu likiwa na maana ya chombo maalumu cha kuonesha muda au wakati. Mara nyingine neno ‘saa’ linapotumiwa, humaanisha ‘muda’ au ‘wakati’.

Kwa mara ya kwanza katika historia, neno hili –saa lilianza kutumiwa katika nchi za Ujerumani na Ufaransa mnano Karne ya 16 Baada ya Kristo, japo kiitikadi linaonekana kutumika kabla ya hapo. Katika historia ya dunia, mtu wa kwanza kugundua kifaa hiki alikuwa ni Peter Henlein raia wa Ujerumani.

Jina hili ‘saa’ au ‘watch’ kwa Kiingereza, lilitokana na neno wæccan lenye maana ya “kuwa macho, amka”, wæcce –“ulinzi” au wæccende – “kubakia macho”.

Kimsingi, neno hili lilitumika katika mazingira ya kubadilishana kwa zamu za walinzi katika nchi za Magharibi. Katika utamaduni wa Waswahili, matumizi ya saa yalikuja enzi za ukoloni.

Kabla ya ujio wa wageni, kwa kufuata mzunguko wa dunia kwenye jua, jamii nyingi za Waswahili zilikuwa zinatumia mfumo wa kutaja majira ya siku kama vile macheo/machweo, jua la utosi, na giza/usiku.

Hakukuwa na mfumo wa saa kama huu uliopo sasa. Baada ya ujio wa wakoloni, mfumo wa saa katika lugha ya Kiswahili ulikuwa ukiandikwa katika mfumo wa lugha za kigeni. Hata Waswahili wenyewe walikuwa wakitamka saa tofauti na inavyoandikwa.

Kwa mfano, saa 3:00 pm ilitamkwa kama saa tisa alasiri, saa 12:01 am ilitamkwa kama saa sita usiku na kadhalika. Saa za mwanzo kugunduliwa zilikuwa ni saa za mezani, ukutani, mfukoni na mikononi. Saa zilizozoeleka ni zile zinazotumia numerali (namba), doti/nuktapacha au namba za Kirumi zinazotumia akarabu.

Akarabu ni mshale katika uso wa saa unaoonesha ama saa, dakika au sekunde. Wakati mwingine, akarabu hutumika kuonesha uzito katika mizani au upande fulani katika uso wa dira.

Hivyo, katika baadhi ya aina za saa kuna akarabu tatu ambazo fupi zaidi huonesha saa, ile ndefu na pana huonesha dakika na ile ndefu nyembamba huonesha sekunde. Akarabu zote hizi zinapokamilisha mzunguko mmoja hukamilisha sekunde sitini, dakika moja au saa moja.

Aidha, zaidi ya saa zinazotumia akarabu, kuna saa zinazotumia mlishio wa nuktapacha kuhesabu sekunde, dakika au saa. Namna ya kusoma na kutamka saa kwa Kiswahili Kadri muda ulivyosonga, aina mbalimbali za saa ziliendelea kutengenezwa na kuuzwa katika jamii za Waswahili.

Mpaka sasa, kuna aina nyingi za saa zinazotumika katika jamii hizo. Kwa mfano, bado kuna saa zinazovaliwa mikononi, za mezani, ukutani na za kwenye vitumi (simu, aipadi na kompyuta).

Kutokana na maendeleo ya lugha ya Kiswahili na Waswahili wenyewe, kwa sasa usomaji na uandikaji wa saa umebadilika na kuboreka zaidi. Badala ya kusoma na kuandika saa 3:00 pm alasiri katika mfumo wa kigeni, kwa sasa huandikwa 9:00 alasiri, saa 12:01 am usiku huandikwa 6:01 usiku na kadhalika. Kwa ufafanuzi zaidi angalia jedwali lifuatalo:

MSIMU mpya wa Ligi Kuu ya England 2020/2021 umeanza na ...

foto
Mwandishi: John M.

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi