loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

TLP kumnadi Magufuli kampeni kuelekea uchaguzi Oktoba

CHAMA Cha Tanzania Labour (TLP) kimeazimia katika kampeni za uchaguzi mkuu wa Oktoba mwaka huu kuzunguka nchi zima kueleza kwa kina miradi iliyotekelezwa na Serikali chini ya Rais John Magufuli.

Hayo yalisemwa jana Jijini Arusha na Katibu Mwenezi wa TLP Taifa, Geofrey Stephen katika mkutano na waandishi wa habari akiwa na viongozi wa chama hicho ngazi ya Mkoa wa Arusha. Stephen alisema kuwa TLP haitaweka mgombea urais kwa kuwa kinaamini kwa asilimia 100 kuwa mgombea wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Rais Magufuli ni chaguo tosha kuendelea kuongoza nchi hii.

Mwenezi huyo alisema kuwa Rais Magufuli amefanya mambo mengi katika nchi hii katika muda wa miaka mitano aliyoongoza, hivyo anapaswa kuchaguliwa tena kuongoza miaka mitano mingine ili aweze kukamilisha miradi mingine aliyoanzisha kwa maslahi ya Watanzania wote.

‘’Sisi TLP katika kipindi cha kampeni tutazunguka nchi zima kumnadi Rais Magufuli ili aweze kuchaguliwa tena kuongoza nchi hii na ndio maana hatutaweka mgombea urais kwa sababu chama chetu kinamkubali mgombea wa CCM bila ya kipingamizi,”alisema.

Aidha wanachama na viongozi wa TLP kote nchini wameendela kuwapongeza Mwenyekiti wa chama hicho taifa, Agustine Mrema kwa kuchaguliwa tena kuwa Mwenyekiti wa chama hicho na Makamu wake Dominata Rwechungura na Zanzibar Husein Juma.

Naye Katibu wa TLP Mkoa wa Arusha, Kinanzaro Geofrey alieleza kuwa chama hicho Mkoa wa Arusha kitasimamisha wagombea kwenye majimbo yote na nafasi za udiwani. Alisema mfano mzuri wa chama hicho kwa jimbo la Arusha mjini pia kitasimamisha mgombea kwani historia inaonesha wagombea wote waliotoka TLP ni bora, hata mbunge wa sasa wa Chadema, Godbless Lema ni zao la chama hicho.

Alisema wapo wanachama wa vyama vingine wanaofanya vizuri wote wametoka ndani ya chama hicho, hivyo wanajipanga kuona wanazalisha wanasiasa ambao watasaidia nchi kufikia malengo yenye tija kwa nchi.

MGOMBEA Urais wa Chama ...

foto
Mwandishi: John Mhala, Arusha

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi