loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

TBS yajipanga kuhakikisha vipimo vyote nchini vipo sahihi

MKURUGENZI Mkuu wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS), Dk Yusuf Ngenya amesema shirika hilo limejipanga kuhakikisha wafanyabiashara wanaozalisha bidhaa zao nchini wanatumia vipimo sahihi ili waweze kupata bidhaa zenye ubora kwa matumizi ya Watanzania na nje ya nchi.

Dk Ngenya alitoa kauli hiyo jijini Dar es Salaam juzi na wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na maadhimisho ya Siku ya Vipimo Duniani. Maadhimisho hayo hufanyika kila mwaka Mei 20, ambapo kwa mwaka huu kauli mbiu imebeba ujumbe usemao; “Vipimo katika Biashara za Kimataifa”

“Sisi kama shirika tukishirikiana na taasisi nyingine zenye dhamana ya kushughuka na vipomo tumejipanga kuhakikisha kila mfanyabiashara anazalisha bidhaa yake hapa kwetu Tanzania anatumia vipimo sahihi ili kupata bidhaa zenye ubora,”alisema Dk Ngenya.

Alisema vipimo ni huduma muhimu sana katika ufanyaji biashara, ujenzi na uendeshaji wa viwanda vinavyotoa bidhaa bora.

“Nawashauri wamiliki wa viwanda wote hapa nchini na wafanyabiashara mtumie vipimo sahihi au kupata huduma ya upimaji kutoka kwa taasisi zinazofanya vipimo ili tuweze kufanyabiashara kimataifa kwa urahisi na kukuza uchumi wetu,” alisema Dk Ngenya.

Alifafanua kwamba biashara ya kimataifa inaweza kufanyika kwa urahisi iwapo uzalishaji katika viwanda vyetu utafanyika kwa kuzingatia vipimo sahihi vilivyopo katika kila kiwango cha bidhaa husika.

Aliongeza kwamba vipimo vinagusa maisha yetu ya kila siku akitoa mfano akisema; “Unapoenda kununua mahitaji yako ya kila siku, uwe mchele, mkate au mafuta, unahitaji kipimo iwe ni kwa uzito, au kwa ujazo.”

Aidha alisema hata huduma za hospitali, zinapatikana kwa vipimo vya uchunguzi kugundua tatizo na kupewa dawa zilizozalishwa kwa kipimo sahihi na kupaswa na kutakiwa kuzitumia kwa kipimo sahihi.

Aliendelea kusisitia umuhimu wa vipimo kwamba unapojaza upepo au kukaza nati za gari lako, unahitaji kipimo kwa usalama wa maisha yako na ya wanaotuzunguka hivyo alisema:”Ni muhimu sana kuhakikisha unapata huduma hizi na nyinginezo kwa kutumia vipomo sahihi.”

MGOMBEA Urais wa Chama ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi