loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

SENZO: TUNAANGALIA KUMALIZA TUKIWA KILELENI

KLABU ya Simba imesema kwa sasa inaangalia zaidi jinsi itakavyorejea katika Ligi Kuu Tanzania Bara na Michuano ya Kombe la Shirikisho (ASFC) na kumaliza kileleni na sio suala la usajili.

Hayo yalisemwa jana na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Simba, Senzo Mazingiza alipozungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam kuhusu mipango mbalimbali ya klabu hiyo.

Alisema kuwa ligi bado haijaisha, hivyo kwa sasa mawazo yao yote ni kuangalia jinsi watakavyorejea katika Ligi Kuu Tanzania Bara na Kombe la Shirikisho na kutwaa ubingwa.

Bingwa wa Ligi Kuu huwakilisha Taifa katika Ligi ya Mabingwa wa Afrika wakati yule wa Kombe la Shirikisho la Azam, hushiriki katika michuano ya Kombe la Shirikisho.

Akizungumzia wachezaji wao wa kimataifa watarejea lini, Mazingiza alisema amekuwa amekuwa akiwasiliana mara kwa mara na mara ya mwisho ilikuwa jana (juzi) na watakaporejea ndio ataujulisha umma.

“Nimekuwa nikiwasiliana na wachezaji wetu walio nje pamoja na makocha na jana tu (juzi) nilizungumza na Meddie Kagere, Francis Kahata (pichani) , Clatous Chama, Sharaf Shiboub pamoja na makocha na meneja wa timu, “alisema Mazingiza.

Pia alisema Tanzania ndio imefunga anga lake lakini nchi ambazo wachezaji hao wanatoka mipaka yao haijafunguliwa hivyo hawawezi kusema chochote hivyo kwa vile timu za soka zimeruhusiwa kuanza mazoezi huenda zikawakosa wachezaji wake waliopo nje ya nchi.

Alisema kuwa wachezaji wote wenye mkataba na Simba wataendelea kuwa chini ya klabu hiyo na hawana mpango wowote wa kuwaachia, hivyo kwa sasa hawezi kuzungumzia kuacha au kusajili wachezaji wengine.

KIUNGO mshambuliaji wa Yanga, Bernard Morrison amejiunga na Simba kwa ...

foto
Mwandishi: Rahel Pallangyo

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi