loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Simba, Mo Dewji watoa msaada Muhimbili

KLABU ya Simba jana imetoa msaada wa lita 1000 za sabuni na vipukusi kwa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), Taasisi ya Mifupa Muhimbili (MOI) na Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI), Dar es Salaam jana.

Msaada huo ambao uliambatana na uzinduzi wa sehemu za kunawia mikono umetolewa na klabu hiyo kwa ushirikiano na MO Dewji Foundation.

Akizungumza wakati wa kukabidhi msaada huo Ofisa Mtendaji Mkuu wa Simba, Senzo Mazingiza alisema klabu yao inajivunia kuwa karibu na jamii hasa kipindi hiki cha kukabiliana na janga la corona kwa kutambua umuhimu na kazi kubwa inayofanywa na watoa huduma za afya.

“Sisi tunajivunia kuwa karibu na jamii na ndio maana tunajaribu kusaidia kupambana na janga hili la corona maana bila watu hakuna soka pia tunatambua mchango wa watoa huduma za afya,” alisema

Pia alisema wanajivunia kuwa klabu ya mfano kwa timu za Ligi Kuu Tanzania Bara kusaidia kupambana na janga la corona maana walitoka kugawa barakoa kwa wananchi na sasa wamekuja kwenye taasisi zinazotoa huduma kwa umma.

Naye Mkurugenzi wa Tiba Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), Dk Hedwiga Swai aliishukuru kwa msaada huo na kuomba wahisani wengine kujitokeza kusaidia maana wana mahitaji mengi kuliko kuachia serikali pekee.

“Tunashukuru kwa msaada huu, umekuja wakati muafaka wakati serikali inapambana kuhakikisha inatokomeza janga la corona na njia pekee ya kupambana na corona ni kunawa mikono kwa sabuni na maji yanayotiririka,” alisema Dk Swai.

Naye Mkurugenzi wa MO Dewji Foundation, Babra Gonzalex, alisema ujenzi wa sehemu ya kunawia ilifanyika mwezi Machi na wanaendelea katika hospitali nyingine za Mloganzila, Mwananyamala, Amana na Temeke.

Hafla hiyo pia Mkurugenzi wa udhibithi wa ubora wa huduma za afya ya moyo, JKCI, Tulizo Shemu, Mkurugenzi wa Tiba wa MOI, Dk Samuel Swai na Ofisa habari wa MNH Aminiel Aligaesha, alisema sabuni zote zitapelekwa katika mageti ya kutokea na kuingia ila vipukusi vitagawanywa katika taasisi zote tatu.

KIUNGO mshambuliaji wa Yanga, Bernard Morrison amejiunga na Simba kwa ...

foto
Mwandishi: Rahel Pallangyo

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi