loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Coastal yasema Mwamnyeto hayuko sokoni

COASTAL Union imesisitiza Bakari Mwamnyeto bado ni mchezaji wao na ana mkataba wa mwaka mmoja wa kuitumikia klabu hiyo.

Kauli hiyo imetolewa jana na Mwenyekiti wa timu hiyo, Steven Mguto akikanusha taarifa zinazosambaa kuwa Simba na Yanga zimeanza kufanya mazungumzo na mchezaji huyo.

“ Mwanyeto bado ana mkataba na Coastal wa mwaka mmoja hivyo hayupo sokoni kwa kuuzwa na hadi sasa hakuna timu iliyofika kwetu kuonesha nia ya kutaka kumsajili,” alisema.

Alisema hivi karibuni wamesikia taarifa kwenye vyombo vya habari kwamba timu kadhaa zimeanza kufanya mazungumzo wanafuatilia kupata ushahidi kujua kama ni kweli ili kuzishtaki kwanini zinavunja utaratibu kwa mchezaji mwenye mkataba.

“Sisi tunasikia kwenye vyombo vya habari timu za Simba na Yanga zinafanya mazungumzo naye tukipata ushahidi tutazichukulia hatua za kisheria kwa kuvunja kanuni za mchezo wa soka,” alisema Mguto

Alisema kama kuna timu inamuhitaji basi waende kufanya mazungumzo na uongozi na kama mchezaji atakuwa tayari basi watafanya biashara.

BAADA ya Namungo FC ...

foto
Mwandishi: Tuzo Mapunda

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi