loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Man UNITED hawana corona, waanza mazoezi

WACHEZAJI wa Manchester United juzi Jumatano kwa mara ya kwanza walianza mazoezi ya pamoja baada ya vipimo vya wachezaji wote kutoka na kuonesha hawana maambuikizi ya ugonjwa wa Covid-19.

Haya ni mazoezi ya pamoja ya mara ya kwanza baada ya kupita miezi miwili, mara ya mwisho kushuhudiwa nyota hao wakifanya mazoezi katika Uwanja wa Carrington ilikuwa Machi 13.

Timu zimeanza kufanya mazoezi kufuatia klabu za Ligi Kuu England kupiga kura ya ndio kuridhia wachezaji waanze mazoezi ya kujiandaa na ligi ambayo inatarajiwa kuendelea hivi karibuni.

Timu zote 20 za Ligi Kuu zilikubaliana kuanza mazoezi ndani ya wiki hii na kila moja imeanza kujiandaa kwa aina yake. Nahodha wa timu hiyo, Harry Maguire alikuwa wa kwanza kufika katika viunga vya Carrington Jumatano asubuhi akiwa pamoja Fred, Scott Mc- Tominay na NemanjaMatic.

Makinda wa timu hiyo nao walikuwepo katika mazoezi, akiwemo Angel Gomes, Mason Greenwood na Tahith Chong baada na wao kupewa taarifa za kuhitajika mazoezini.

Kiungo Paul Pogba, Bruno Fernandes pamoja na OdionIghalo wao walishindwa kuwasili asubuhi na badala yake walionekana majira ya mchana pamoja na Sergio Romero wakiwa na barakoa zao.

Taarifa zinaeleza kwamba kutakuwa na awamu tatu za mazoezi kulingana na kuwasili kwa wachezaji, ambapo wamepangiwa viwanja vitano, ambao wapo watakaoanza kwa dakika 40 kuwapima utimamu wao wa mwili.

Taarifa za awali zilieleza kwamba wachezaji sita tu ndio waliokutwa na maambukizi ya corona kutoka klabu 19 zilizopima wachezaji wake, Norwich bado hawajatoa majibu ya vipimo vyao.

ERIC Nshimiyimana amekubali mkataba mpya na sasa ataendelea kuwa Kocha ...

foto
Mwandishi: MANCHESTER, England

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi