loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Hofu yamuondoa Kante mazoezini

UONGOZI wa klabu ya Chelsea umempa ruhusa kiungo wake N’golo Kante kutofanya mazoezi baada ya mchezaji huyo kukumbwa na hofu ya ugonjwa wa Covid 19 unaosababishwa na virusi vya corona.

Awali, kiungo huyo wa kimataifa wa Ufaransa alionekana akijumuika na wenzake katika mazoezi Jumanne hii akiwa na muonekano mpya wa nywele kichwani kwake lakini ameshindwa kuendelea na mazoezi.

Licha ya uongozi kukubali kumpa ruhusa hiyo, lakini haijawekwa wazi ni lini atarejea mazoezini. Inaonekana kwamba Kante hajakaa sawa kiakili baada ya tukio lake la kuanguka ghafla akiwa katika mazoezi na wachezaji wenzake wa Chelsea miaka miwili ilioyopita.

Alifanyiwa vipimo vya afya hakuonekana kama ana tatizo kwenye moyo wake na alishiriki vema Michuano ya Kombe la Dunia iliyofanyika Urusi, 2018. Chelsea ni moja kati ya timu, ambazo zinajali utu kwa wachezaji wake ambao kipindi hiki ligi imesimama iliwaruhusu wachezaji wake wote wa kigeni kurudi nchini mwao kukaa na familia zao.

Mchezaji mwingine aliyekosa mazoezi ni Callum Hudson-Odoi taarifa za kutokuwepo kwake hazijawekwa wazi, inaaminika ni mgonjwa lakini sio wa Covid 19 wala si hofu ya tukio lake la kutuhumiwa kubaka.

ERIC Nshimiyimana amekubali mkataba mpya na sasa ataendelea kuwa Kocha ...

foto
Mwandishi: CHELSEA, England

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi