loader
Dstv Habarileo  Mobile
20 Percent aja na filamu ya Mama Neema

20 Percent aja na filamu ya Mama Neema

MSANII wa muziki wa kizazi kipya, Abbas Kinzasa ‘ 20 Percent’ amesema wimbo wa Mama Neema ni kisa cha kweli ila haihusiani na yeye ila anakuja na fi lamu ya pili ya Mama Neema.

Akizungumza jana, 20 Percent, ambaye aliwahi kuvuma na wimbo wa Mama Neema aliotoa mwaka 2007 alisema wimbo huo aliutengenezea filamu baada ya kuona nyimbo zake hazipigiwi kwenye vyombo vya habari.

“Ule wimbo wa Mama Neema ni stori ya ukweli japo hainihusu mimi moja kwa moja, Neema ni mkubwa na anajiheshimu pia anasifa kama za Monalisa japo kwa sasa yupo nchini Rwanda” alisema 20 Percent.

“Nakuja na filamu ya pili ya Mama Neema, itaonesha Neema alivyotoroshwa na mama yake mdogo kwenda Rwanda, kipindi naiachia ile filamu zilivumishwa stori kuwa nilikataza nyimbo zangu zisipigwe kwenye vyombo vya habari ndiyo maana nikazihamishia kwenye ile filamu,” alisema 20 Percent. 

Alisema mwanamke aliyeimba naye wimbo wa ‘Ningekusamehe’ alikuwa mpenzi wake na walizaa mtoto mmoja na amebarikiwa watoto wa kutosha bila kutaja idadi. 20 Percent amewahi kuvuma na nyimbo nyingi kama Bange Bange, Maisha ya Bongo, Binti Kimanzi, Yanini Malumbano, Money Money na nyingine.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/f1e76194c5d49ff3f637089a2d8ecf7d.jpg

YANGA leo inashuka katika Uwanja wa Benjamin ...

foto
Mwandishi: Rahel Pallangyo

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi