loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Waziri Mkuu mpya wa Lesotho aapishwa

WAZIRI Mkuu mpya wa Lesotho, Moeketsi Majoro(pichani) ameapishwa kushika wadhifa huo baada ya kujiuzulu kwa aliyekuwa akishika nafasi hiyo, Thomas Thabane (80).

Uamuzi wa kujiuzulu kwa Thabane Mei,19, mwaka huu ulitokana na shinikizo kuhusu kesi inayomkabili yeye na mkewe mpya, ya kuhusishwa kwenye mauaji ya mkewe wa zamani mwaka 2017.

Hata hivyo, wote wawili walikana tuhuma hizo za mauaji. Waziri Mkuu huyo mpya aliwahi kuwa Waziri wa Fedha nchini humo. Kuapishwa kwake juzi kulihudhuriwa pia na Thabane Akizungumza wakati akijizulu, Thabane alisema ameamua kujiuzulu kutokana na umri wake na pia familia yake inahitaji kuwa naye karibu.

Kwamba ametumikia nchi hiyo kwa muda wa kutosha na sasa ni wakati mzuri wa kupumzika. Akila kiapo cha kushika wadhifa huo mkubwa, Majoro alisema atakuwa mkweli na mwaminifu na anaomba Mungu amsaidie. Awali kabla ya uteuzi huo, alikuwa akifanya kazi kwenye Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF).

Mke wa zamani wa Thabane, Lipolelo Thabane (58) aliuawa mwaka 2017 siku mbili kabla ya Thabane hajaapishwa kuwa waziri mkuu. Kifo chake kilitokana na kupigwa risasi kadhaa nje ya nyumba yake.

Wakati huo wanandoa hao walikuwa wametengana kabla ya kutalikiana. Tukio hilo lilileta taharuki na hofu nchini humo. Miezi miwili baadaye, Thabane alioa mke mwingine, Mesaiah Thabane (43), ambaye anadaiwa kuwa ndiye mpanga mpango wa mauaji ya Lipolelo.

Mesaiah anashtakiwa kwa tuhuma ya mauaji ya mama huyo na yuko nje kwa dhamana. Wakati anaapishwa kuwa waziri mkuu juzi, Maesaiah hakuwepo kwenye sherehe hizo na mumewe. Thabane aliomba radhi mambo yote yaliyotokea wakati wa utawala wake akiwa waziri Mkuu.

“Nilifanya kazi kwa uwezo wangu kuwatumikia watu wa Lesotho. Inawezekana upande mwingine sikufanya vizuri wakati wa utawala wangu kama waziri mkuu. Naomba mnisamehe kwa makosa yangu,” Thabane.

WAZIRI wa Nchi Ofi si ya Rais, Tawala za Mikoa ...

foto
Mwandishi: MASERU, Lesotho

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi