loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Nyumba ya Abeid Karume iliyopo Mwera yakarabatiwa

SERIKALI ya Mapinduzi ya Zanzibar( SMZ) imeanza kuzitambua na kuzifanyia ukarabati mkubwa nyumba za kihistoria za viongozi wakuu waasisi wa Zanzibar, ikiwemo Rais wa kwanza wa Zanzibar, hayati Abeid Amani Karume (pichani) iliyopo Mwera.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamo wa Pili wa Rais, Mohamed Aboud alisema hayo wakati akifafanua kuhusu mikakati ya kutunza historia za viongozi wakuu walioleta ukombozi wa Zanzibar.

Alisema tayari kazi hiyo imeanza, baada ya kutungwa sheria ya kuwalinda viongozi wakuu wa nchi na kupitishwa na wajumbe wa Baraza la Wawakilishi.

Alisema nyumba aliyozaliwa Rais wa kwanza wa Zanzibar, hayati Abeid Amani Karume iliyopo Mwera imeanza kukaratabiwa. Lakini, alisema ukarabati wa nyumba hiyo umekwama kutokana na Chama cha Mapinduzi (CCM) kusema kazi hiyo itafanywa na wao, ambao ndiyo dhamana.

‘’Nyumba ya makumbusho iliyopo Mwera wenzetu wa Chama cha Mapinduzi walisema wataifanya wao kutokana na umuhimu wake na mchango wa kiongozi huyo katika harakati za ukombozi wa Mapinduzi ya Zanzibar,’’alisema.

Alitaja nyumba nyingine ambayo imeanza kufanyiwa ukarabati ni ile iliopo Mwembeladu, ambayo ndiyo chimbuko la kuanzishwa kwa chama kilicholeta ukombozi cha ASP. Alisema serikali imeanza kutekeleza sheria ya kuwalinda na kuwatunza wastaafu walioleta ukombozi, ikiwemo Shehe Thabit Kombo na Pili Khamis.

Aidha, kaburi la Rais mstaafu wa Zanzibar, Shehe Idriss Abdul Wakil limefanyiwa ukarabati na kuwekewa uzio na ndugu walishirikishwa na kutoa ushauri.

‘’Sheria hiyo tayari imeanza kufanya kazi kwa kuyatunza makaburi ya waasisi wa mapinduzi na viongozi wastaafu, akiwemo Makamu wa Rais na Waziri Kkiongozi mstaafu marehemu Dk.Omar Ali Juma,”alisema.

RAIS John Magufuli ametoa wito kwa ...

foto
Mwandishi: Khatib Suleiman, Zanzibar

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi