loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Kaya 311 zazingirwa na maji ya Ziwa Tanganyika

KAYA 311 katika vijiji 14 vya kata sita za Halmashauri ya Wilaya Uvinza mkoani Kigoma, zimeathirika baada ya nyumba zao, kuzingirwa na maji na baadhi kubomoka, kutokana na kujaa kupita kiasi kwa kina cha ziwa Tanganyika.

Mkuu wa Wilaya ya Uvinza, Mwanamvua Mrindoko alisema hayo akitoa taarifa kwa Mkuu wa mkoa huo, Emmanuel Maganga wakati wa ugawaji wa misaada mbalimbali ya kibinadamu kwa waathirika.

Mrindoko alisema pamoja na hilo, jumla ya ekari 800 zimeharibiwa kabisa na maji hayo ambayo chimbuko lake ni mvua nyingi zilizokuwa zikinyesha.

Mbali ya kuathiri makazi ya watu, lakini pia maji hayo yameathiri miundombinu ya barabara kwa baadhi ya miti iliyokuwa ikiingia ziwa Tanganyika ambayo maji yamekuwa yakitoka na kurudi barabara na hivyo kuharibu kabisa daraja la mto Lagosa na sehemu kubwa ya barabara ya Ilagala kwenda Kalya kuahithiriwa na maji hayo.

Alisema kati ya kaya 311 zilizoathirika, miongoni mwao watu 116 wameathirika zaidi ya kuhitaji misaada na ndiyo ambao walikuwa wakipatiwa misaada hiyo iliyotolewa na wahisani mbalimbali wakiwao Msalaba Mwekundu Tanzania waliotoa magodoro 100, blanketi 200, ndoo za kuchotea maji 100 na madumu ya kuhifadhia maji 100.

Aliwataja wengine waliotoa misaada hiyo ni Taasisi ya Bilal Muslim Tanzania ikiwakilishwa na Mwenyekiti wake, Mohsin Abdallah Sheni ambao walitoa tani 2.5 za chakula cha aina mbalimbali ikiwemo mifuko 100 ya sukari, mifuko 100 ya saruji huku Kigoma Hiltop ikitoa mifuko 40 ya unga wa sembe.

Aidha, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa ilichangia kiasi cha Sh milioni 2.5 zilizowasilishwa kwenye Kamati ya Maafa na Katibu Tawala wa Mkoa, Rashidi Mchatta huku Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR) wakichangia gari na mafuta kwa ajili ya

RAIS John Magufuli ametoa wito kwa ...

foto
Mwandishi: Fadhili Abdallah, Kigoma

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi