loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Wafanyabiashara wapaza sauti kufurika nyaya 'feki' sokoni

 WAFANYABIASHARA wa vifaa vya umeme jijini Dar es Salaam  wamelalamikia uwepo wa bidhaa zisizokidhi viwango zinazozalishwa hapa nchini na baadhi ya viwanda. 

Wakitolea mfano nyaya, wafanyabiashara hao wameiomba Serikali kupitia Shirika la Viwango Tanzania (TBS) na Tume ya Ushindani (FCC) kufanya msako viwandani na madukani ili kuwabaini wenzao ambao si waaminifu katika sekta hiyo. 

Wakizungumza kwa nyakati tofauti katika maeneo ya Kariakoo, baadhi ya wafanyabiashara hao pamoja na wanunuzi wa bidhaa wanaodai kumekuwepo na wimbi la uzalishaji wa bidhaa hizo hususani nyaya za umeme za majumbani ‘wiring’ zisizo na viwango.

Wafanyabiashara hayo waliojitambulisha kwa majina ya Rashid Salum pamoja na Frank Mtonga waliopo eneo hilo wamesema kuwa bidhaa hizo zinauzwa katika baadhi ya maduka ya Kariakoo, jijini Dar es Salaam na kuwakosesha soko wale wanaouza bidhaa 'original' kwani wateja wanakimbilia zinazouzwa kwa bei ya chini ambazo hazina viwango. 

“Kuna maduka mengi hasa maeneo ya mitaa ya Narungombe na maeneo mengine yanayouza bidhaa hizo...wanauza nyaya ambazo hata ukizitamaza kwa macho utabaini kuwa hazina ubora, kigezo kikubwa kinachofanya wananchi wazikimbile ni unafuu wa bei” alisema Salum. 

Bila kutaja majina ya viwanda vinavyotengeneza nyaya hizo,Salum alisema kimsingi nyaya hizo pamoja na baadhi ya vifaa vingine vya umeme, vinazalishwa kutoka katika viwanda vinavyomilikiwa na raia wa kigeni wasio waaminifu na kuiomba Serikali kufuatilia kwa undani ili kubaini.

Kwa upande wake Mtonga amesema kuwa alishawahi kupokea lawama kutoka kwa baadhi ya wateja wake, waliomtuhumu kuwauzia nyaya zisizo na ubora, suala alilodai kuwa hakulifahamu kwa kuwa hakuwa na uelewa wa kutosha juu ya nyaya hizo na viwango vyake.

Aliiomba TBS kufanya ukaguzi wa mara kwa mara katika maduka pamoja na viwandani  hatua itakayosaidia kuwabaini wahusika kisha kuchukuliwa hatua kulingana na sheria na taratibu za nchi kwa madai kuwa wenye viwanda hivyo wamekuwa wakifanya hayo kwa makusudi licha ya kujua athari za kufanya hivyo.

Akitolea mfano katika suala hilo, Mtonga alisema kwa nyaya zenye ubora wa viwango ambazo zinauzwa kwa wastani wa Sh. 100,000, huuzwa kwa wastani wa hadi 70,000 kwa nyaya zisizokuwa na ubora wa viwango na hivyo kuathiri ushindani wa bei katika soko huku pia zikileta madhara kwa wananchi yakiwemo ya nyumba kuungua.

Kwa nyakati tofauti, Serikali kupitia Waziri wa Nishati Dk Medard Kalemani imekuwa ikisisitiza utumiaji wa vifaa vya umeme vyenye ubora vinavyozalishwa hapa nchini na kupiga marufuku uzalishaji wa vifaa vyote visivyo na ubora.

MGOMBEA Urais wa Chama ...

foto
Mwandishi: Oscar Job

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi