loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Polisi: Tumejipanga Sikukuu ya Eid el-fitri

JESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam kwa kushirikiana na vyombo vingine vya ulinzi na usalama limeeleza kuwa limejipanga kikamilifu kuimarisha ulinzi na usalama katika kipindi cha sikukuu ya Eid el-fitri inayaotarajiwa kuadhimishwa hivi karibuni pindi itapotangazwa na Mufti Mkuu.
Taarifa iliyotolewa leo Ijumaa (Mei 22, 2020) inaeleza kuwa Jeshi hilo limewaasa wananchi wa Jiji la Dar es Salaam kusherehekea sikukuu ya Eid El-fitri kwa amani na utulivu na kujiepusha  na vitendo vya uvunjifu wa sheria kwani limejipanga kuimarisha doria maeneo yote muhimu zikiwemo nyumba za ibada,fukwe za bahari.

"Tunawatadharisha watembea kwa miguu na madereva wa vyombo vya moto kuendelea kufuata sheria za usalama barabarani ikiwa ni pamoja na kuendelea  kutii amri ya serikali ya kupakia abiria kulingana na idadi ya viti vilivyopo ndani ya gari (level seat) na watakaokaidi agizo hilo watachukuliwa hatua kali za  kisheria," imesema taarifa hilo iliyotolewa na Kamanda Lazaro Mambosasa. 
SACP Mambpsasa amewakumbusha waumini wa wa dini zote kujitokeza kwenye nyumba zao za ibada kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa siku tatu (Ijumaa, Jumamosi na Jumapili) kwa jinsi  anavyoendelea  kutuepusha na hili janga la ugonjwa wa COVID 19 kama alivyoelekeza Rais John Magufuli huku akiwahakikishia kuwa "Jeshi la Polisi lipo timamu kuimarisha ulinzi na usalama kwenye nyumba zote za ibada."
Jeshi la Polisi limeshauri wananchi kuendelea kuchukua tahadhari dhidi ya maambukizi ya virusi vya Corona ikiwa ni pamoja na kufuata miongozo inayotolewa na Serikali pamoja na wataalam wa afya.
Hata hivyo SACP Mambosasa Dar es Salaam amewaomba wakazi wa mkoa wa Dar es Salaam kuendelea kutoa ushirikiano kwa kutoa taarifa za uhalifu  kwani jukumu la kuzuia uhalifu ni la kila Mtanzania.

 

BODI ya Michezo ya Kubahatisha nchini kwa kushirikiana na Mamlaka ...

foto
Mwandishi: MWANDISHI WETU

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi