loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

YAMEKWISHA:Tanzania, Kenya zakubaliana namna ya kupima madereva Corona

NCHI za Tanzania na Kenya zimeafikiana kuwa madereva watatakiwa kupimwa ugonjwa unaosababishwa na virusi vya corona katika nchi zao na kupewa cheti maalum kitakachowatambulisha kutokuwa na maambukizi ambacho kitakuwa halali kwa siku 14 pekee.

Baada ya siku hizo kukamilika, madereva hao watalazimika kupimwa tena wakiwa nchini Kenya au Tanzania na endapo watagundulika, watarudishwa katika nchi zao.

Hayo yameelezwa leo na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isaac Kamwele leo, Ijumaa, mpakani Namanga baada kumalizika kikao kilichomjumuisha Waziri wa Uchukuzi wa Kenya, James Macharia.

Kukutana kwa mawaziri hao na hatimaye kufikia makubaliano hayo kumetokana na mazungumzo yaliyofanyika hivi karibuni kwa njia ya simu baina ya Rais John Magufuli na Uhuru Kenyatta wa Kenya.

Akiwa mkoani Singida, Rais Magufuli alibainisha kuwa wameshamaliza sintofahamu hiyo hivyo ilikuwa ni suala la watendaji wa serikali zote mbili kukutana. 

foto
Mwandishi: Veronica Mheta

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi