loader
Picha

Kiwanda cha Sukari cha Kilombero chaanza uzalishaji

KIWANDA cha Sukari cha Kilombero kimeanza uzalishaji wiki mbili mapema kuliko misimu mingine ya nyuma. Kimefanya hivyo ili kusaidia kuziba pengo la upungufu wa sukari lililopo nchini kwa sasa.

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Kiwanda hicho, Joseph Rugaimukamu wakati wa kikao kuangalia hali ya upungufu wa sukari kiwandani hapo. Kikao hicho kilikuwa kati ya Mrajis wa Vyama vya Ushirika na Mtendaji Mkuu wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika (TCDC), Dk Benson Ndiege, viongozi wa vyama vya wakulima wa miwa wa Bonde la Kilombero na uongozi wa Kiwanda cha Sukari cha Kilombero.

“Kiwanda cha Sukari Kilombero kwa mwaka huu kimeanza uzalishaji wiki mbili mapema kuliko tarehe za kawaida za uzalishaji kutokana na hali ya upungufu wa sukari uliopo nchini” alisema Rugaimukamu.

Alisema kiwanda kimelazimika kufanya hivyo, ili kuongeza bidhaa hiyo sokoni na kuitikia wito wa Serikali wa kusaidia upatikanaji wa sukari kwa wananchi na kwa bei nafuu. Alisema mwaka huu, lengo la kiwanda ni kuzalisha tani 127,000 za sukari.

Akizungumza katika kikao hicho, Mrajis wa Vyama vya Ushirika na Mtendaji Mkuu wa Tume hiyo, Dk Benson Ndiege, alisema Tume imeweka mikakati ya usimamizi wa uvunaji miwa, kwa lengo la kuondokana na changamoto katika vyama vya ushirika. Alisema , mkakati na usimamizi huo ni kuona ni namna gani kuweza kuvuna miwa kwa wakulima ili kukabiliana na upungufu wa sukari nchini.

“Nia ya serikali ni kujitosheleza kwa sukari, naomba kiwanda muendelee na juhudi za kuongeza uzalishaji wa sukari ili kuongeza kiwango cha upatikanaji wa bidhaa hiyo muhimu katika jamii,” alisema Dk Ndiege.

Mwenyekiti wa Kidatu Amcos, Bakari Idd, kwa niaba ya viongozi wenzake, alisema kuwa wanashindwa kuvuniwa miwa yote inayozalishwa na wakulima, hali inayochangia kushindwa kulipa madeni yao, waliokopeshwa na benki kwa ajili ya kujikwamua kiuchumi.

WANANCHI wa kisiwa cha Pemba  visiwani Zanzibar wamepongezwa kupambana na ...

foto
Mwandishi: John Nditi, Kilombero

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi