loader
Picha

Wema awalaumu rafiki zake

MWIGIZAJI wa fi lamu na mwanamitindo ambaye kwa sasa anaendesha kipindi cha Mapishi cha Pika na Wema, Wema Sepetu amesema watu wake wa karibu ndio waliokuwa wakimfanya apoteze tumaini katika maisha yake.

Wema ambaye mara nyingi rafiki zake wa karibu, akiwemo mama yake mzazi wamekuwa wakimlalamikia sana kuhusu makundi ya marafiki zake kumpotosha, amesema kwamba kuna wakati mtu unaweza kujiuliza wapi anakosea na ukajilaumu sana kwa makosa, ambayo hata wewe mwenyewe huwezi kuelewa.

Alisema amekuwa akijiuliza sana bila majibu, ambapo amegundua kuwa watu ambao wanaweza kuwa ni watu wake wa karibu sana, ndio wamekuwa wakimuangusha.

“Tunapaswa kusonga mbele na kutoangalia nyuma, huwa inakua ngumu sana kurudi nyuma, lakini hatupaswi kukata tamaa,” alisema.

SERIKALI baada ya kufanya kikao na wadau wa michezo imesema ...

foto
Mwandishi: Mohamed Mussa

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi