loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Wawakilishi wahimizwa kutoa elimu ya corona

WAJUMBE wa Baraza la Wawakilishi wametakiwa kuendelea kutoa elimu ya kupambana na ugonjwa wa COVID 19, ambao husababishwa na virusi vya corona katika majimbo ya uchaguzi ili wananchi wawe salama na kuendelea na kazi za ujenzi wa taifa.

Hayo yamesemwa na Naibu Spika wa Baraza la Wawakilishi, Mgeni Hassan Juma wakati akiwakabidhi Wawakilishi barakoa ambazo zimetokana na fedha walizochanga kwa ajili ya kuwasaidia wapiga kura wao.

Alisema Zanzibar imepiga hatua kubwa ya kupambana na ugonjwa wa covid-19 kwa sababu wananchi wake wamekuwa wakifuata masharti ya kujikinga na maambukizi mapya.

Hassan aliwataka wawakilishi kuzisambaza barakoa hizo na kuzifikisha kwa wapiga kura wao kwa malengo yaliyokusudiwa.

“Barakoa hizi zinatokana na fedha zetu tulizochanga kwa ajili ya kuwasaidia wapiga kura katika majimbo ya uchaguzi ili wawe salama na maambukizi mapya,” alisema.

Hassan alisema barakoa hizo, pia wamewakabidhi wajumbe watatu wa Baraza la Wawakilishi wanaotoka katika vyama vya upinzani, baada ya kutambua mchango wao mkubwa wa kuishauri serikali.

“Wapo wenzetu wawakilishi watatu kutoka katika vyama vya upinzani, ambao nao tumewapa barakoa hizi ili wakazikabidhi kwa wanachama wao,” alisema.

Wawakilishi hao ni Waziri wa Afya Hamad Rashid, Waziri asiye na Wizara maalumu Juma Ali Khatib na Said Soud. Mapema, Mnadhimu wa Baraza la Wawakilishi aliwapongeza wajumbe wa Baraza la Wawakilishi kwa kuonesha moyo wa ujasiri kuchangia mapambano dhidi ya ugonjwa wa covid 19.

“Nimefurahishwa sana na juhudi za wajumbe wa Baraza la Wawakilishi kutoka Chama cha Mapinduzi kwa kukubali kuchangia shilingi milioni 33 na kutengeneza barakoa ambazo leo hii tunawakabidhi kwenda kutumiwa na wapiga kura wetu,” alisema na kuongeza kuwa zitasambazwa katika majimbo ya uchaguzi Unguja na Pemba.

Mwakilishi wa Kuteuliwa na Rais, Juma Ali Khatib aliwapongeza wajumbe wa Baraza la Wawakilishi kutoka CCM kwa kuonesha mapenzi na kutambua mchango wa wajumbe kutoka upinzani.

WAZIRI wa Maji Jumaa Aweso amesema maeneo mengi ...

foto
Mwandishi: Khatib Suleiman

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi