loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

'Vijana limeni zabibu mtoke kimaisha'

MMLIKI wa kiwanda cha kutengeneza mvinyo cha Alko Vintages, kilichopo Dodoma, Archard Kato amepongeza jitihada za Serikali ya Awamu ya Tano za kuboresha mazingira ya uwekezaji na kutoa rai kwa vijana kutumia fursa zilizopo hasa katika kilimo hasa cha zabibu kujikwamua kiuchumi.

Alitoa kauli hiyo mbele ya Waziri wa nchi Ofisi ya Waziri ya Mkuu anayeshughulikia Uwekezaji, Angellah Kairuki wakati alipofanya ziara kiwandani hapo kujionea shughuli mbalimbali za uzalishaji na kusikiliza changamoto.

“Vijana lazima mjiamini na kuwa na uthubutu katika kuanzisha biashara ili kuingia kwenye sekta ya uwekezaji, hakikisha una maono au jambo linalokuvutia na weka mikakati ya kulifikia,”alisema Kato.

Alko Vintages Co. Ltd kinazalisha mvinyo wa aina mbalimbali ikiwemo Dompo, Altar, St Mary’s, Image, Rose na Klymax. Akizungumza kwenye ziara hiyo ya kukagua shughuli za uzalishaji katika viwanda vinavyozalisha mvivyo kikiwemo pia cha Domiya Estate kinachozalisha vinywaji vikali na baridi kama soda, maji na chai baridi aina ya Asante, Kairuki alisema kuwa serikali ina mipango na mikakati ya kuhakikisha kuwa kuna mazingira bora ya uwekezaji.

“Serikali inatambua changamoto mnazopitia na imeweka mikakati ya kuhakikisha inazitatua ikiwemo uanzishwaji wa sheria mpya ya uwekezaji nchini inayolenga kuweka mazingira bora ya uwekezaji,” alisema Waziri Kairuki.

Alisema, changamoto ambazo wawekezaji wamekuwa wakikabiliana nazo zinaendelea kutatuliwa ikiwa ni pamoja na; utitiri wa kodi, ukosefu wa maji ya uhakika, ubovu wa miundombinu ya barabara, gharamza kubwa za uzalishaji, uzalishaji duni kwa ubora na wingi wa zabibu, ukosefu wa aina mabalimbali za zabibu.

Changamoto nyingine walizobainisha ni ugumu wa kuanzisha viwanda vidogo vya kusindika zabibu, ukosefu wa utaalamu katika kilimo cha zabibu, pamoja na uwepo wa bidhaa zisizo na ubora sokoni.

Akijibu changamoto hizo, Waziri Kairuki aliwatoa hofu kwa kuainisha maeneo muhimu yaliyofanyiwa maboresho ikiwa ni pamoja na kufutwa kwa tozo na kodi zaidi ya 168 nchini, kuendelea kuboresha miundombinu muhimu ikiwemo barabara zinazosimamiwa na Tarura, kuwa na uhakika wa upatikanaji wa umeme na maji ili kila mwekezaji na mfanyabiashara anufaike na uwekezaji wake.

Waziri huyo pia aliwataka wawekezaji kuvitumia vyema vyombo vya habari katika kutoa elimu na kujitangaza ili kuendelea kuwa na soko la uhakika kwa kuzingatia ubora wa bidhaa wanazozalisha.

KATIBU Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Leonard Akwilapo, ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Maalumu, Dodoma

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi