loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Wawakilishi wapongezwa, bajeti Juni 15

RAIS wa Zanzibar, Dk Ali Mohamed Shein amewapongeza wajumbe wa Baraza la Wawakilishi kwa kuendesha vikao vya baraza vyenye mijadala iliyojikita kulenga maslahi ya wananchi ambao ndiyo wapiga kura wao.

Akizungumza katika hotuba ya Baraza la Eid, aliwataka wananchi kujitayarisha kusikiliza hotuba ya bajeti ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa mwaka wa fedha 2020/21 itakayosomwa na Waziri wa Fedha na Uchumi Juni 15, mwaka huu.

Alisema kinachofanywa na wajumbe wa Baraza la Wawakilishi ni kutekeleza masharti ya kikatiba yanayowataka kuendelea na vikao vya Baraza kwa ajili ya kupitisha bajeti ya Serikali na Wizara zake zote.

Alisema amekuwa akifuatilia kwa karibu michango ya wajumbe wa Baraza la Wawakilishi katika kuisimamia serikali na kupitisha bajeti za Wizara na kuridhishwa kwa kiasi kikubwa.

“Natoa pongezi za dhati kwako weye binafsi Spika wa Baraza la Wawakilishi pamoja na wajumbe wako kwa kutekelza majukumu ya kikatiba ya kuwasilisha bajeti za Wizara mbali mbali na serikali katika kipindi hichi kigumu cha ugonjwa wa Covid-19 unaosababishwa na ugonjwa wa corona,” alisema.

Alisema anampongeza Spika wa Baraza la Wawakilishi, Zubeir Ali Maulid kwa kuendesha mkutano wa Baraza la Wawakilishi huku wakiweka mbele maslahi ya taifa na wananchi.

Alisema bajeti ya serikali kwa mwaka wa fedha 2020/21 inatarajiwa kusomwa ifikapo Juni 15, mwaka huu ambapo aliwataka wananchi kusikiliza mambo muhimu ya mipango ya nchi inayotarajiwa kutekelezwa ambayo imelenga maslahi ya wananchi na maendeleo.

Mkutano wa Baraza la Wawakilishi ambao ulianza Mei 6, mwaka huu tayari wajumbe hao wameshapitisha makadirio mapato na matumizi ya wizara nane.

Kwa mujibu wa taarifa ya Ofisi ya Baraza la Wawakilishi uhai wa Baraza hilo unatarajiwa kuhitimishwa Juni 19, mwaka huu ambapo Rais wa Zanzibar DkAli Mohamed Shein anatarajiwa kulihutubia Baraza hilo kwa ajili ya kuashiria kulivunja tayari kwa maandalizi ya Uchaguzi mkuu mwezi Oktoba.

JESHI la Polisi kupitia Kikosi cha Farasi, limeanzisha huduma ya ...

foto
Mwandishi: Khatib Suleiman, Zanzibar

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi