loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Wanawake wauza pombe hatarini corona, ukimwi

WANAWAKE wengi wanaojihusisha na utengenezaji na uuzaji wa pombe za kienyeji katika Wilaya ya Temeke mkoani Dar es Salaam, wapo kwenye hatari kubwa ya kupata maambukizi ya virusi vya ukimwi pamoja na ugonjwa wa Covid -19 unaosababishwa na virusi vya corona.

Uchunguzi wa gazeti hili umebaini kuwa, hatari hii inatokana na uzembe katika kuzingatia masharti ya kujikinga kuambizwa virusi vya corona huku kukiwa na hatari kubwa ya kuambukizwa virusi vya ukimwi.

Imebainika kuwa, hii ni kunatokana na mazingira ya kazi na wateja wao ‘kukumbatia’ ngono zembe na kusahau masharti ya kujilinda dhidi ya corona ambayo ni kuepuka misongamano, kuepuka kugusana kwa kubuana au kushikana mikono, kuepuka unyenyevu wa hewa kutoka mdomoni au puani kwa mtu mwingine na kunawa mara kwa mara kwa kutumia maji tiririka na sabuni au kutumia vitakasa mikono.

Kwa nyakati tofauti, gazeti hili limetembelea eneo la Majimatitu lililopo Mbagala Kuu, Temeke Sterio na Buza karibu na Davis Corner wilayani Temeke katika Jiji la Dar es Salaam.

CORONA INAVYOWANYEMELEA

Katika maeneo hayo ya kuuzia pombe za kienyeji, gazeti hili hakuona uwepo wa maji tiririka katika kwa ajili ya wauzaji na wateja kunawa mikono. Hili, ni tofauti na maelekezo yanayotolewa na serikali kuwa kila penye mikusanyiko, yawepo maji tiririka na sabuni au vitakasa mikono.

Aidha imebainika kuwa, kutokana na udogo wa vyumba vya kuuzia pombe hizo kumekuwa na ukaribu mkubwa zaidi kati ya watoa huduma na wateja wao tofauti na maelekezo yanayowataka watu kukaa angalau umbali wa mita moja.

Mwandishi wa makala haya kwa muda aliokuwa akifuatilia mienendo ya maisha katika eneo hilo kwa siku mbili akiwa amevaa barakoa, katika chumba kimoja cha kuuzia pombe hizo za kienyeji alionekana tofauti na wengine kwani ndiye pekee aliyekuwa amevalia barakoa hali iliyowafanya wengine kumtazama kwa mshangao.

Hata katika siku ya pili alipokaa kwa takribani dakika 45 kuanzia saa 3 usiku katika eneo la nje kidogo ya eneo la kuuzia, pia hakuona mteja wala muuzaji akiwa amevaa barakoa, wala kuwa na kitakasa mikono.

HATARINI KUPATA HIV

Ufuatiliaji wa kina wa siku tatu uliofanywa na gazeti hili kwa nyakati tofauti za usiku ukihusisha njia za mahojiano na ufuatiliaji wa mienendo ya wauzaji wa pombe hizo dhidi ya wateja umebaini kuwapo kiwango kikubwa cha matukio ya ngono zembe.

Aina kubwa ya pombe inayouzwa ni gongo ambapo kutokana na kutokana na uhalisia wa biashara yenyewe kuhusisha asilimia kubwa ya watu wa kiwango cha chini cha maisha, wengi wao hawana taarifa za na elimu ya kutosha mintarafu kujikinga dhidi ya maambukizi ya VVU, kwani wauzaji na wanunuzi wengi katika kata hizo, hawazingatii matumizi ya kinga wakati wa kujamiiana.

Katika Kata ya Majimatitu, gazeti hili liliwaona wauzaji wanawake wakiwa kwenye ukaribu zaidi wa kimapenzi na wateja wao hao.

Aidha, lilishuhudia muuzaji mmoja akiondoka kwenda kwenye sehemu ya jirani kwa ajili ya kuchepuka’. Kupitia mazungumzo na watu mbalimbali, imebainika kuwa wanawake wanaouza pombe za kienyeji, wengi hujirahisisha na ‘kujiachia’ kwa wanywaji pombe kama njia ya kuvutia na kuwashikilia wateja wa pombe zao wasihamie pengine.

Mwandishi aliyejifanya mteja akiwa na mwenyeji wake eneo hilo la kuuza pombe za kienyeji, alizungumza na mteja huyo kujua kama alitumia kinga (kondomu) alipokuwa na mwanamke huyo muuzaji pombe, alisema:

“Dah! Kaka, nimeteleza kisela,” akimaanisha kuwa amefanya ngono zembe.

Kijana huyo aliyejulikana kwa jina la Ally, ni mume mtu na baba wa mtoto mmoja; anasema anapenda kwenda mahali hapo kwani anawapata kirahisi wanawake wengi wanaouza pombe hizo za kienyeji.

Mmoja wa wauzaji wa pombe hizo, Mariam Magendagenda (si jina halisi) anabainisha kuwa, asilimia kubwa ya wauzaji wa pombe hizo wanaendekeza ngono kutokana na mapato kidogo yatokanayo na biashara hiyo, pia elimu ya kujilinda dhidi ya maambukizi ni ndogo na hawajawezeshwa kujikinga.

Anabainisha kuwa, yeye licha ya kuuza aina hizo za pombe, amekuwa akijilinda dhidi ya ngono zembe kutokana na elimu aliyopewa na wadau wa masuala ya ukimwi.

Anasema: “Kinachosikitisha ni kuwa tunaotengeneza pombe, ndio siye pia tunaouza na tunaowahudumia wateja hawa hivyo inakuwa rahisi kwa wengine kukubali matakwa ya wateja hata hata yaliyo hatari maana hakuna namna vinginevyo, wateja watakukimbia…”

Anasema: “Ninashaurii wadau waendelee kutoa elimu sahihi kwa wauza pombe wenzangu kuhusu namna ya kuepuka maambukizi haya ya virusi vya ukimwi likiwamo kubwa la kujiepusha na mambo ya ngono zembe maana tunauza pombe, hatuuzi miili na pia, kama kwa mfano wanawake wauza pombe wakiwa na kondomu, ikitokea ‘anatoka na mtu’, basi watumie hizo kinga…”

Gazeti hili liliwasiliana na Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Kukabiliana na Unyanyasaji wa Kijinsia, Sophia Komba anabainisha kuwa shirika lake limekuwa likiwafikia wanawake mbalimbali wilayani Temeke na kuwaelimisha namna ya kujilinda.

Anasema mbali na kuwapatia kinga na kuwaelewesha namna ya kukwepa vishawishi pia shirika lake limewatahadharisha dhidi ya athari zinazoweza kujitokeza pindi wakiendekeza ngono zembe.

Kwa mujibu wa Komba, mara nyingi kwenye miradi mikubwa ya kimaendeleo kumekuwa na mwingiliano mkubwa wa watu wakiwamo wanaopendelea unywaji pombe zikiwamo za kienyeji na baadhi yao ni waathirika.

Alisema wametoa elimu hiyo kwa wauzaji wa pombe za kienyeji walio pembeni mwa ujenzi wa mradi wa Mabasi ya Mwendokasi unaojengwa Mbagala, lakini pia Barabara ya Mtwara kwenda Newala.

FIGO ambayo jukumu lake kubwa ni kuchuja damu na kutoa ...

foto
Mwandishi: Evance Ng’ingo

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi