loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

TBC yaombwa kuonesha FDL, SDL

SHIRIKA la Utangazaji la Tanzania (TBC), limeombwa kuangalia uwezekano wa kutangaza moja kwa moja mechi za Ligi Daraja la Kwanza (FDL) na Ligi Daraja la Pili (SDL).

Kauli hiyo ilitolewa na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk Harrison Mwakyembe, wakati wa mkutano wake wa waandishi wa habari hivi karibuni jijini Dodoma alipokuwa akizungumzia hatua za usalama zinazopaswa kufanywa wakati shughuli za michezo zinaanza tena kutoka Juni 1 mwaka huu.

"Wakati wa mikutano yetu tumekuwa na wadau mbalimbali kabla ya kuanza tena kwa ligi za mpira wa miguu, tuligusa pia kwenye suala la matangazo.

"Sote tunajua kuwa Azam TV ni watangazaji rasmi wa Ligi Kuu Bara na Kombe la Shirikisho la Michezo ya Azam (ASFC) na wanafanya kazi nzuri lakini kama serikali, tumezungumza na TBC ili kuangalia uwezekano wa kutangaza moja kwa moja mechi za FDL na SDL kuwapa Watanzania burudani zaidi ya mpira wa miguu,” alisema Dk Mwakyembe.

Aliongeza kuwa kuna mambo mengi yanajitokeza katika ligi hizi za madaraja ya chini ambaoz mashabiki wanastahili kutazama.

LIONEL Messi, alifunga bao lake la 700 katika historia yake ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi